Monday, June 24

WATU WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 27 KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA YA MILIONI 32

0


Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WATU wanne wakazi wa jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 27 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo la kupatikana na vipande sita vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 15000 ambazo ni zaidi ya Sh. Milioni 32.5

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa gari aina ya Funcargo yenye namba za usajili T.540 DDS ambayo ilitumika kubebea meno ya Tembo hayo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Maria Kasonde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi 11 ulioletwa na upande wa mashtaka pamoja na vielelezo viwili katika kuthibitisha kesi hiyo.

Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni Solomon Mtenya, Siasa Athumani, Musa Ligagabile, Omary Sabo.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 31 iliendeshwa na mawakili wa Serikali, Salum Msemo na Constantine Kakula. Akisoma hukumu Hiyo, Hakimu Kasonde amesema, “Mahakama imeridhika na ushahidi wa uliotolewa na upande wa mashtaka na mahakama inawahukumu kutumikia kifungo  cha miaka 27 gerezani ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akifafanua adhabu hizo, Hakimu Kasonde amesema, katika shtaka la kwanza washtakiwa Mtenya, Athumani na Sabo, wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani huku

katika shtaka la pili la kujihusisha na nyara za serikali washtakiwa wote wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani. Aidha katika shtaka la tatu la kusafirisha nyara hizo, washtakiwa  wote wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani.

Hata hivyo, Mahakama imesema kuwa adhabu zote hizo zitaenda kwa pamoja hivyo watuhumiwa wote watakaa gerezani kwa miaka 20 pekee.

Katika kesi hiyo, watuhumiwa wanadaiwa, Juni 23, 2016 huko Kimara, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa wakisafirisha vipande sita vya meno ya tembo vya USD 15,000 ambazo ni sawa na shilingi 32,565,000.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2wf3chW
via

logoblog

Thanks for reading WATU WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 27 KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA YA MILIONI 32

Share.

Leave A Reply