Sunday, August 25

WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA – DKT. GEORDAVIE KASAMBALE

0


Na Woinde Shizza  wa Michuzi TV, Arusha

Watanzania dumisheni amani na upendo  uliopo  katika nchi yetu kwani ndio zawadi  pekee tulioachiwa na mwenyezi Mungu, amesema Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako Dkt. Geordavie  Kasambale (pichani) jijini hapa wakati akiongea na waumini Wa kanisa hilo katika ibada ya Chuo cha Manabii kilichopo Kisongo.  

Alisema kuwa Watanzania tunayo amani ambayo tumezawadiwa na Mungu hivyo ni wajibu wa kila MTU kuienzi, kuidumisha   pamoja na kuilinda.

“Unajua Mungu anatupendelea sana Watanzania. Ametupa amani ya nchi yetu…ametufanya tunaishi kwa upendo. Hebu  angalieni nchi zingine wanapigana kila siku… Kuna vita ndugu kwa ndugu hawapendani. Lakini sisi Watanzania tunaishi kwa amani hivyo ni vyema amani hii tuliopewa tuilinde kama vile mboni ya jicho letu” alisema Geordavie

Aidha aliwataka Watanzania kutoruhusu mtu yeyote yule kuingilia amani yetu na kuivuruga kwani hii ni zawadi ya pekee tuliopewa na mwenyenzi Mungu. Pia alimtaka kila Mwananchi kupitia imani yake kuendelea kuombea  nchi yetu ya Tanzania iendelee  kuwa na amani, na pia aliwakumbusha kuwaweka viongozi wetu wa kitaifa akiwepo Rais wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania katika maombi kila siku ili mungu aendelee kuwaongoza na kuwapigania.

Dkt. Kasambale amewataka Watanzania kutii Sheria za nchi bila vurugu, huku akisisitiza wanasiasa kutopandikiza chuki miongoni mwa wananchi badala yake wawaunganishe na kuwafanya kitu kimoja.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2ICmiGQ
via

logoblog

Thanks for reading WATANZANIA DUMISHENI AMANI TULIYOJAALIWA – DKT. GEORDAVIE KASAMBALE

Share.

Leave A Reply