Thursday, February 21

VIDEO: Diamond Atangaza Mikoa Ambayo Wasafi Festival itafanyika, Alikiba Aalikwa

0


Kampuni ya Wasafi imetangaza kuanza rasmi kwa tamasha la Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24, mwaka huu mpaka Desemba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 5, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Diamond Platnumz, amesema kwa kuanzia tamasha hilo lenye kauli mbiu ya ‘Mchezo usiuchezee wewe Kabisa’ litafanyika mkoani Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.


Diamond alitaja mikoa mingine itakayofuata kuwa ni Iringa ambapo litafanyika Novemba 30 na kufuatiwa na Morogoro na mikoa mingine itatangazwa hapo baadaye huku Nairobi likitarajiwa kufanyika Desemba 31 mwaka huu


VIDEO:DOWNLOAD APP YETU YA MASAMA BLOG HAPA👇👇👇ILI UWE UNAPATA HABARI HIZI KIRAHISI

Share.

Leave A Reply