Saturday, August 24

Serikali imeonya kwa baadhi ya watu wataotaka kuharibu operesheni ya mifuko ya Plastiki.

0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
 Serikali  imesema kuwa katika operesheni ya kuondosha mifuko ya plastiki baadhi ya watu wamejipanga kukwamisha kwa operesheni.

Hayo ameyasema Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa wamejipanga vizuri katika operesheni na kutaka wananchi  kutoa ushirikiano.
Amesema  kuwa  wazalishaji wa mifuko wamekuwa na nguvu kubwa na kufanya wananchi kuwa sehemu ya watu wanaolalamika huku wakionekana  hakuna kitu wanachonufaika kutokana na mifuko hiyo.
Waziri Makamba amesema kuwa kuna viwanda vitatu vimejitokeza kuchukua mifuko  ya plastiki kwa ajili ya kuzalishia mabomba pamoja na madawati.
Amesema Baraza la  Taifa la Ma Mazingira pamoja  na wizara zingine wamejipanga katika uondoshaji wa mifuko ya plastiki.
Aidha amesema kuwa nchi nyingi zimepita katika uondoshaji wa mifuko ya plastiki hivyo Tanzania si nchi ya Kwanza kufanya zoezi hilo ambalo lina changamoto zake lakini Serikali imejipanga vizuri.
“Katika zoezi hili kuna watu baadhi watajitokeza katika kutaka kukwamisha  lakini hawatafanikiwa kutokana na elimu iliyotolewa na waliopata uelewa wawe mabalozi wa kuendelea kuelimisha  wananchi”. amesema Makamba
Nae Mwanasheria  wa Baraza la Mazingira (NEMC) Manchare Heche amesema kuwa wadau mbalimbali wamepewa elimu juu ya uondoshaji wa mifuko ya plastiki.
Amesema kuna mifuko inaruhusiwa katika vifungashio hivyo mifuko mingine ikiwemo mifuko laini hairuhusiwi na mtu binafsi ikikutwa na mifuko hiyo faini no she. 200000 na kiwanda ni sh.milioni tano na kuendelea.
Amesema  kuwa sheria zipo pamoja na kanuni zake hivyo hakuna mtu ambaye ataonewa kwa watu watakaokwenda kinyume na sheria ya mazingira katika mifuko ya plastiki.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira January Makamba akizungumza na Wahariri na Waandishi Habari Waandamizi katika semina ya kuwajengea uelewa wa operesheni ya uondoshaji wa mifuko ya plastiki ambayo itaanza rasmi Juni Moja Mwaka huu iliyofanyika katika Ofisi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) jijini Dar es Salaam.

 Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Manchare Heche akionesha baadhi ya mifuko ambayo itaendelea kuwepo katika vifungashio ikiwemo katika mifuko ya saruji pamoja na sehemu za ujenzi katika mafunzo ya wahariri na waandishi wa Habari Waandamizi iliyofanyika katika Baraza hilo jijini Dar es Salaam.

 Afisa Mazingira Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Ndimbumi Joram akizungumza na wahariri na waandishi wa habari waandamizi kuhusiana na madhara ya mifuko ya plastiki katika Semina iliyofanyika katika Baraza hilo jijini Dar es Salaam.

Baadhi wahariri na waandishi habari waandamizi wakipatiwa mafunzo kuhusiana na mifuko ya plastiki katika Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) jijini Dar es Salaam.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2W0r4jN
via

logoblog

Thanks for reading Serikali imeonya kwa baadhi ya watu wataotaka kuharibu operesheni ya mifuko ya Plastiki.

Share.

Leave A Reply