Monday, August 19

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA TCRA KUTOZIFUNGA LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA

0Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amesema mchakato wa kusajili laini za simu kwa kuunganisha na Kitambulisho cha Taifa(NIDA) usogezwe mbele hadi Desemba mwaka huu huku akiagiza Watanzania wasiokuwa na vitambulisho vya NIDA wasihukumiwe kwa laini zao kufungiwa.

Kabla ya kauli hiyo ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo Aprili 26,2019 akiwa mkoani Mbeya ,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) walitangaza kuwa watazima laini za simu ambazo hazitakuwa zimesajiliwa na kuunganishwa na NIDA kwa kuweka alama ya kidole kigumba ambapo pia walitangaza kuanza kwa usajili wa laini za simu kuanzia tarehe moja ya mwezi ujao.

Akizungumza leo akiwa ziarani mkoani Mbeya pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amezungumzia usajili wa laini za simu uliotangazwa na TCRA ambapo amesema hakuna sababu ya kuwahukumu Watanzania kwa kuzima laini zao za simu kwa kigezo kwamba hawajasajili laini za simu.

Amesema ifahamike si kwamba anazuia usajili wa laini kwani ni muhimu na usajili huo una faida zake na ni nyingi lakini amefafanua Tanzania kuna Watanzania zaidi ya milioni 50 na wenye vitambulisho vya NIDA hawafiki milioni 15.

Hivyo amesema ni vema TCRA waongeze muda wa kusajili laini za simu kwa kwenda sambamba na utoaji wa vitambulisho vya Taifa. “Watu wasihukumiwe kwa kutosajili simu kwasababu ya NIDA.Mchakato uende pamoja ili watazania wasiopata wasihukumiwe,” amesema Rais Magufuli .

 

Amesisitiza kadri NIDA wanavyotoa vitambulisho ndivyo kasi yake iendane na usajili wa laini za simu,hivyo wasifungue laini kwa kipindi hiki kwani kufanya ni sawa na kuwahukumu Watanzania.

Wakati huo huo Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuanza kuchunguza upya madai ya mtoto wa miaka minne wa kiume kulawitiwa.Rais ametoa maagizo hayo baada ya mmoja aliyekuwa katika mkutano wa Rais kupata nafasi ya kuzungumza mbele take ambapo alitoa malalamiko ya mtoto wake kulawitia.

Mama huyo baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza amemwambia Rais Magufuli kuwa mtoto wake wa kiume amelawitiwa na sasa anajisaidia muda wote na baada ya kitendo hicho aliamua kwenda kwenye vyombo vya ulinzi na usalama lakini hadi sasa haana msaada wowote zaidi ya kuzungushwa.

Amesema kuwa amekwenda kuonana na Kamanda wa Polis Mbeya,Mkuu wa Jeshi la Polisi ncbini IGP pamoja na Jaji Mkuu lakini anaona anazungushwa tu,hivyo matumaini yake yamebaki kwa Rais Magufuli ambaye ni Rais wa wanyonge.

“Rais wangu naomba msaada wako,nimekwenda kila mahali hadi kwa Jaji Mkuu,nisaidie mheshimiwa Rais ,nyaraka za note ambako nimekwenda ninazo.Mtoto aliyelawitiwa ni mwanaume na picha yake ninayo,lakini kwenye makaratasi wanasema ni mwanamke,” amesema mama huyo wakati anamuleza Rais.

Hata hivyo Rais alimuuliza kama amekwenda na mtoto huyo mkutano hapo lakini mama huyo akajibu ameshindwa kwenda naye kwani anajisaidia Mara kwa mara,hivyo hakuweza kufika naye

Kutokana na maelezo hayo Rais Magufuli alimhakikishia mama huyo kuwa uchunguzi utafanyika na haki itatendeka ambapo ameomba nyaraka akabidhiwe mwanasheria ili kuanza ufuatiliaji.

Pia Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha mama huyo hasumbuliwi huku akimpa fedha kwa ajili ya kujikimu na mtoto wake.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2VwvIcU
via

logoblog

Thanks for reading RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA TCRA KUTOZIFUNGA LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA

Share.

Leave A Reply