Wednesday, August 21

'PROFESA' JUMA BHALO ALIYETIKISA KWA TAARABU

0


Na: Moshy Kiyungi

Juma Bhalo alikuwa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa taarab Afrika ya Mashariki.

Mohammed Khamis Juma Bhalo, ndiyo yaliyokuwa majina yake japokuwa alipewa umaarufu kama Profesa Juma Bhalo.Nguli huyo alizaliwa mwaka 1942 huko Shela eneo la zamani la mji wa zamani Mombas, Kenya.Bhalo aianza kuimba taarabu tangu mwaka 1957, lakini mwaka uliofuatia wa 1958 alianzisha kikundi chake kilichoitwa Bhalo and Party huku akisaidiana na malenga wa Mvita.

Profesa Bhalo alikuwa ni mwenye asili ya Mombasa, sifa nyingi alijizolea kufuatia uwezo wake mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo za taarabu.Nyimbo hizo zilikuwa na mashairi yaliyobeba ujumbe mzito kwa jamii. Bhalo alikuwa nauwezo wa kuimba huku akipigia kinanda.

Juma Bhalo pi alijaaliwa kipaji cha kukariri nyimbo za Kihindi na kuziimba pasipo kukwama.Mtandao mmoja wa mawasiliano ulizungumza na kitinda mimba wa marehemu Profesa Juma Bhalo, anayefahamikia kwa jina la Ahmed Juma, kutoka Mombasa.

Alieleza kuwa baba yake baada ya kuugua kwa muda mrefu Bhalo akafariki Aprili 05, 2014 akiwa na umri wa miaka 74.Siku iliyofuatia ya Aprili 06, 2014 alilazwa kwenye nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya Kikoani, huko Mombasa.

Ahemed Juma alipoulizwa juu ya mtoto ambaye ameweza kufuata nyayo za baba yake Profesa Juma Bhalo.Alisema ilikuwa vigumu sana kwa baba yake kukubali mwanawe kufuata nyayo zake japokuwa baadaye alimkubalia miongoni mwa wanawe hao kufuata nyayo hizo.

Yeye mwenyewe alikiri kutoielewa zaidi historia ya maisha ya mzazi wake Profesa Juma Bhalo.Anachojuwa kuwa Bhalo hakuweza kuendelea na masomo hivyo aliishia darasa la 4, na kuendeleza masomo ya madrasa, hakuweza kumaliza masomo ya elimu ya msingi kwa kuwa wazazi wake walishindwa kulipa karo ya shule.

Mwaka 1957 Bhalo alihamia Mombasa na kupata kazi Forodhani. Akiwa Mombasa alikutana na kushirikiana na wanamuziki wa taarabu wa Mombasa.Hakuipenda sana kazi ya Forodha hivyo mwaka 1959, akahamia katika mji wa Tanga kwa mjomba wake, na huko akajiunga na kundi maarufu la Taarab wakati ule lililoitwa Young Nverty.

Akiwa na kundi hilo Bhalo alipata ujuzi mkubwa wa muziki wa Taarab.

Mwaka 1966, alirejea kwao Malindi kwa muda mfupi. Hatimaye akarejea tena Tanga mwaka 1962 na kaapiga Taarab na kundi la Young Stars Taarab.

Mwaka 1966 alirudi Mombasa na kuanzisha kundi la Bhalo and Party, kundi amabo alidumu nalo mpaka mauti yake yalipomfika. Mwaka 2007 baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuwemo katika muziki wa Taarab. Juma Bhalo ambaye wapenzi wake walimpachika jina bandia la Profesa.

Profes Bhalo alistaafu kazi hiyo kwa maneno yafuatayo “Waswahili wasema kiwate kitu kabla hakijakuata. Kwa hivyo kama mulivyo nishuhudia usiku huu nilivyo natumbuiza kama kawaida yangu, basi leo hii usiku huu kabla hawajajaa watu wakasema ahahhh Bhalo ashazeeka hawezi tena kuimba hivyo najiuzulu ningali bado niko fiti. Kwa hivyo siimbi tena hadharani kikazi. Nawashukuru kwa ushabiki wenu na musijali Mungu akiniwezesha Kasseti mpya nitawaleteya…”

hayo kutokana na ugumu wa hali ya maisha wakati huo.

Baadhi ya nyimbo alizopiga wakati wa uhai wake zlikuwa za Pete, Napenda Moyo wangu spendi mtu, Hukutaka tuwe sote, Tunakupenda wewe tuuuhamu hunishi.Utamu wa kupenda, Asiye juwa kurai si mlezi wa mahaba, Ewe Harufu ya Nuni Na Ewe Uliye Jituza, niliona ni tende kumbe si tende ni mende, Mahaba udhia na Kasha langu

Profesa Juma Bhalo ameacha wajane wawili, watoto 14 japokuwa alibahatika kupata watoto 17 lakini watatu wametangulia mbele ya haki.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba: 0874331200 na 0767331200.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2EGMxZ8
via

logoblog

Share.

Leave A Reply