Sunday, August 25

Mtoto mchanga wa siku mbili atupwa katika Choo cha shule ya sekondari ya kazima manispaa ya tabora

0


Na Editha Edward wa Michuzi Blog, Tabora

Maiti ya mtoto mchanga anaekadiriwa kuwa na umri wa siku mbili amekutwa kwenye choo cha wasichana katika shule ya sekondari Kazima iliyopo manispaa ya Tabora na kusababisha taharuki kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo 

Akizungumza na Michuzi Blog katika eneo la tukio mara baada ya kuvunja choo hicho mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa Bi.Vailleth Machechu amekemea kitendo hicho cha kikatili kilichofanywa mkoani humo.

Aidha mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya kazima Bw. Mrisho Kuvuluga amesema kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa kimefanywa na wananchi kutoka nje ya shule kutokana na kichanga hicho kuonekana na umri wa siku mbili na shuleni hapo utaratibu wa kupima ujauzito wanafunzi wa kike unafanywa kila  msimu wa masomo.

 Wauguzi wakiandaa mwili wa kichanga hicho baada ya kuuopoa chooni

Choo cha wasichana katika shule ya sekondari Kazima manispaa ya Tabora kilipokutwa kichanga hicho. Picha na Edith Edward

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Dk5CQ0
via

logoblog

Thanks for reading Mtoto mchanga wa siku mbili atupwa katika Choo cha shule ya sekondari ya kazima manispaa ya tabora

Share.

Leave A Reply