Thursday, July 18

Msikie hapa Msami Akiongelea Mahusiano Aliyowahi Kuwa Nayo na Irene Uwoya.

0


Msanii wa miondoko ya dansi, Msami amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwanadada Irene uwoya kipindi cha nyuma baada ya mwanadada huyo kuachana na mume wake.

Akijibu swali katika ‘interview’ ya Friday Night Live (FNL) inayorushwa na ETV juu ya kupungua kwa umaarufu wake pamoja na kuondolewa katika listi ya wasanii wanaozungumzwa kuwa ni watanashati baada ya kuachana na Irene Uwoya, Msami amesema

“Wakati mwingine sio kila kitu lazima ukilete katika mitandao, mimi nina bahati ya kuwa na watoto wazuri tuu na hiyo ni kawaida yangu. Anapotoka mtoto mzuri anaingia mtoto mzuri lakini sio lazima tuwe tunatoa taarifa,” amesema. “Ninachotakiwa kukileta hapa ni mziki wangu, kama natoa mziki mzuri na watu wanaupenda basi hayo maisha mengine ya mapenzi ni yapo tuu kila siku,” ameongeza.


Pia msami amezungumzia juu ya tabia ya wasanii wa Bongo Fleva hivi sasa kubadilisha sana staili yao ya mavazi katika majukwaa huku staili yao ya uimbaji ikibaki kuwa ileile. “Sio mabaya kupendeza kwenye ‘show’ kwasababu ni moja ya sanaa ya kuwavuta watu lakini kitu kikubwa ambacho watu wanakosea ni pale wanaposhindwa kuelewa kuwa shabiki anapokuja kwenye show amekuwa ameshakuona kwenye video jinsi unavyovaa kwahiyo anategema kuona ‘perfomance’ yako, na sio kwa maana ya kucheza tuu, perfomance ina vitu vingi sana”. Msami ametambulisha video yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Lingoma’ ambayo ameiachia rasmi wiki hii.

DOWNLOAD APP YETU YA MASAMA BLOG HAPA👇👇👇ILI UWE UNAPATA HABARI HIZI KIRAHISI

Share.

Leave A Reply