Thursday, August 22

MSAKO WA WEZI WA BETRI YA KUWASHIA TAA ZA BARABARANI MJINI TABORA WAANZA

0


Na Editha Edward wa Michuzi Blog, Tabora

Zaidi ya shilingi Milioni Tatu zimetumika  kununua betri ya mashine ya kuongozea taa za barabarani iliyoibwa katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini mkoani Tabora na kusababisha adha kubwa. 


Akithibitisha hilo, Kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora mjini Afande John Mfinanga amesema msako wa kuisaka betri hiyo umeanzishwa na yeyote atakayekutwa nayo mkono mrefu wa sheria utamshughulikia.

Kamanda huyo ametanabahisha kwamba kila mwananchi anatakiwa awe mlinzi wa mali za umma ili kuweza kurahisisha kuwabaini na  kuwafikisha wahalifu kwenye vyombo husika ili kuweza kuimarisha usalama wa mali za umma na watu katika jamii.

“Unapoiba vifaa vya barabarani sio kwamba unaikomoa serikali bali pia unakomoa wananchi wote. Ni vyema tushirikiane kuwafichua wezi hawa kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu”, amesema Afande Mfinanga 

Mkuu wa kitengo cha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Bw.  Raphael Mlimaji amesema wizi wa betri hiyo umesababisha kusimama kwa kutumika taa katika eneo hilo na kusababisha foleni zisizo lazima pamoja na ongezeko la ajali.

“Hii hasara imesababishwa na mtu mmoja lakini inaathiri wananchi wengi sana. Tutaendeleaje wakati nchi inataka kusonga mbele lakini kuna wachache wanaotaka kuturudisha. Hili jambo sio tu  nyuma ni kinyume Cha sheria bali pia limekera wengi na kutia hasara serikali”, amesema Mlimaji.

Aidha Kamanda wa usalama barabarani  Afande Ame Malawi amewataka wananchi mkoani Tabora kufuata Sheria za barabarani ili kuweza kusaidia kuondokana na ajali za Mara kwa Mara.

  Kamanda wa jeshi la polisi wilaya ya Tabora mjini Afande John Mfinanga 

 Nguzo na mashine ya taa za barabarani katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini

Taa za barabarani katika makutano ya barabara ya Isevya katika wilaya ya Tabora mjini

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2VfyWle
via

logoblog

Thanks for reading MSAKO WA WEZI WA BETRI YA KUWASHIA TAA ZA BARABARANI MJINI TABORA WAANZA

Share.

Leave A Reply