Sunday, August 25

Mhasibu UDART afikishwa kizimbani kwa tuhuma za mkughushi Tiketi

0


Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MHASIBU  wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Alphonce Kika (29), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa akikabiliwa na mashtaka 36 ya  kughushi tiketi zenye namba tofauti tofauti za mabasi ya mwendo kasi.

Mshtakiwa Kika anayeishi Mabibo, Loyola amesomewa shtaka lake leo Aprili 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wa Mahakama hiyo na kusomewa mashtaka 36 ya kughushi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janeth Mugho akisaidiana Jenifa Masue amedai, mshtakiwa ametenda makosa hayo Aprili 4, 2019 katika Kituo cha mabasi ya mwendo kasi kilichopo Mbezi ndani ya Wilaya ya Ubungo na jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa siku ya tukio mshtakiwa Kika  kwa nia ya kudanganya au kutapeli alighushi tiketi 36 za basi zenye namba tofauti tofauti za Aprili 18, 2019 akidanganya kuwa zimetolewa na UDART kitu ambacho si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mshtaka yote na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana amhapo mahakama imemtaka kuwa na  mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh milioni 20.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13,2019, kwa mujibu wa upande wa mashtaka  upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

MHASIBU wa Kampuni ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) ,Alphonce Kika ,akisindikizwa na polisi kuelekea katika  kizimba cha  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa ajili ya kusomewa mashtaka 36  ya kugushi yanayomkabili .

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Y0wzjT
via

logoblog

Thanks for reading Mhasibu UDART afikishwa kizimbani kwa tuhuma za mkughushi Tiketi

Share.

Leave A Reply