Thursday, August 22

MAGANGA: TUTACHEZA KWA NIDHAMU DHIDI YA MTIBWA SUGAR HAPO KESHO HUKU TUKIISAKA ALAMA 3 MUHIMU.

0


 Na Agness Francis, michuzi Tv. 

MABINGWA  wa Afrika Mashariki na kati Azam fc kesho watashuka dimbani kuvaana na wakatamiwa wa Morogoro Mtibwa Sugar katika mchezo wa 37  mzunguko wa pili Ligi soka Tanzania bara. 

Afisa habari na msemaji wa klabu ya Azam fc Jaffary Maganga amezungumza leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mtanange huo Utapigwa katika dimba la uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa mbili usiku. 

“Baada ya kupoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Simba kwa kutoka  suluhu ya bila kufungana sasa tunashuka tena dimbani kuwakaribisha  Mtibwa Sugar ambapo tunajua kuwa ni timu kongwe na yenye uzoefu iliyopo ligi kuu muda mrefu”amesema Jaffary. 

Maganga amesema kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani kwao hivyo wanahitaji kucheza kwa utulivu na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanashinda gemu hiyo. 

“Tunakumbuka mchezo wa kwanza Mtibwa walifanikiwa mutufunga mabao 2-0 Sasa na sisi tutapambana  kutafuta ushindi wa nyumbani ukizingatia walimu walipata nafasi nzuri ya kuweza kuandaa timu kwa muda mrefu”amesema Msemaji huyo. 

Aidha ameeleza kuwa kikosi chao hakina majeruhi wachezaji wote wako fiti wapo tayari kwa ajili ya kupambania ushindi mnono wa alama 3 wakiwa nyumbani.

Azam anashuka dimbani akiwa nafasi ya 3 alama 69 akiwa ameshacheza michezo 36,huku yanga wakiwa juu yao kwa alama 83 wakiwa na michezo sawa, ambapo wekundu wa msimbazi Simba akiwa kinara wa Ligi kuu soka Tanzania bara akiwa na alama 88 na michezo 35.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2WUt1zm
via

logoblog

Thanks for reading MAGANGA: TUTACHEZA KWA NIDHAMU DHIDI YA MTIBWA SUGAR HAPO KESHO HUKU TUKIISAKA ALAMA 3 MUHIMU.

Share.

Leave A Reply