Monday, August 19

ANAYEFELI SOMO LA ELIMU YA DINI ASIAJIRIWE – ASKOFU RWEYONGEZA

0


Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv.

Serikali Kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeombwa kuangalia upya mtaala wa Elimu, hasa somo la Elimu ya Dini ili kuwafanya Viongozi wajao kuwa waadilifu.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Almachiusi Rweyongeza wa Kanisa la Mt. George Parokia ya Kayanga Jimbo la Kayanga Wilayani Karagwe, katika Ibada ya Pasaka iliyoadhimishwa Kitaifa Jimboni hapo.

Katika Ibada hiyo iliyohudhuliwa na Viongozi Mbalimbali waandamizi  Askofu Rweyongeza amesema Viongozi wamekuwa wakiapa kwa Kutumia vitabu vitakatifu pale waingiapo Madarakani, au Ofisi wanazozisimamia ajabu ni kuwa utendaji wao wa kazi hawamshiriki wala kumtanguliza Mungu, hivyo kwa yule atayekuwa amefeli somo la Dini asiajiriwe popote katika sekta yoyote na Ofisi za Umma.

Aidha ameongeza kuwa Serikali kupitia mfuko wa Kunusuru kaya Maskini, TASAF waangalie upya namna ya mfuko huo kuzisaidia kaya hizo katika suala la afya kwa kuzitafutia bima ya afya badala ya kuwapatia pesa tu.

Akitoa salaam zake kwa Niaba ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesisitiza juu ya suala la Ulinzi na Amani wa mipaka ya Nchi, na wananchi kujiepusha na viashiria vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani hiyo huku akiwataka wale wanoingia Nchini kufuata taratibu za Uhamiaji, na wale wanaofanya biashara za magendo kuacha mara moja na pindi wakibainika hakuna msamaha.

 Askofu Almachius Rweyongeza Wa Kanisa la Mtakatifu George akiongoza Ibada ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika Kayanga Karagwe Kagera.

 Pichani ni Viongozi Wa Serikali , Kushoto Mkuu Wa Wilaya Karagwe Godfrey Muheluka, Naibu Waziri Wa Kilimo, Innocent Bashungwa (MB), Mkuu Wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco E. Gaguti na Katibu Tawala Wa Mkoa Prof Faustine Kamzola wakiendelea na Ibada ya Pasaka katika Kanisa Mt. George Kayanga

 waumini Wa Dini ya Kikirsto wakiendelea na Ibada ya Pasaka, wakisherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo.

Askofu Almachius Rweyongeza akisalimiana na Viongozi Mbalimbali, Ofisini kwake Mara baada ya kuwasili Jimboni hapo kabla ya kuanza kwa Ibada ya Pasaka.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2PloDGI
via

logoblog

Thanks for reading ANAYEFELI SOMO LA ELIMU YA DINI ASIAJIRIWE – ASKOFU RWEYONGEZA

Share.

Leave A Reply