Saturday, July 20

MWANAMKE ANUSURIKA KUFA KWA KUKATWA SIKIO NA MMEWE AKIENDA KANISANI BULIGE – KAHAMA

0Zaituni Said akiwa amekatwa sikio

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zaituni Said (18) mkazi wa kijiji cha Bulige kata ya Bulige katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga amenusurika kufa baada ya kukatwa sikio kwa kisu na mmewe aitwaye Luka Pula.Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jana Novemba 9,2018 majira ya saa tatu usiku wameiambia Malunde1 blog kuwa mwanamme huyo alimvizia mkewe akienda kusali kanisani. 

“Dada huyu ameachana na mmewe kama mwezi mmoja hivi akawa kwao,akiwa kwao akawa kwenye maombi,walikuwa wamefunga,kabla ya kwenda kwenye maombi huyo bwanaake akawa amempigia simu,akamwambia kata simu yako,simu yangu imeishiwa chaji,akaenda kanisani….basi yule bwana akaamua kumvizia kwenye njia ya kanisani akiwa ameshikilia fimbo na kisu akaanza kumchapa na kumkata sikio la mkono wa kulia”….

“Alivyomkata vile akampeleka yeye mwenyewe nyumbani kwao na mwanamke,alivyofika akamwita mama mkwe kisha kaanza kumwelezea mama kuwa amemkuta mwanae kakumbatiwa na wanaume wawili,akaanza tena kumchapa mbele ya mama mkwe huku akimvuta kanga mama mkwe huyo aliyekuwa amevaa kanga moja tu,pakatokea msala mwingine”, 

“Sasa huyo mama mkwe baada ya kuvutwa kanga yake,akashtuka kumuona mwanae anatokwa damu nyingi,akamuuliza vipi,binti akajibu amenitoa na sikio,jamaa akakimbia”, wameeleza.

Wamesema mwanamke huyo alipelekwa katika zahanati ya Wazazi  iliyopo katika kijiji cha Bulige kwa ajili ya matibabu na mtuhumiwa amekamatwa na jeshi la Jadi Sungusungu. 

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa amesema bado hajapata taarifa kuhusiana na tukio anafuatilia taarifa hizo kwa OCD wilaya ya Kahama.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

logoblog

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

Leave A Reply