Sunday, August 25

Mgombea Wa CCM Jimbo La Arumeru Mashariki Apita Bila Kupingwa.

0Msimamizi wa uchaguzi Emmanuel Mkongo amemtangaza mgombea Ubunge (CCM) Dkt.John Danielson Pallangyo kuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa kupita bila kupingwa baada ya Wagombea wenzake 10 kukosa sifa.

Mkongo amesema jumla ya wagombea 11 walichukua fomu na kati yao, watatu hawakurudisha na saba fomu zao zimebainika kutokidhi vigezo.

Amesema wapo ambao hawajalipa fedha ya dhamana ya kugombea ubunge  ya Sh50,000, kukosa wadhamini na kurejesha fomu ya kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako

logoblog

Share.

Leave A Reply