Monday, June 17

UMAARUFU WA MAREHEMU MBUNGE STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJI MAREFU'

0


Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu, atakumbukwa kwa mengi. Pichani akiwaokoa mtu na mtoto wake mara baada ya kuzingirwa na maji ya mafuriko yaliyotokea kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo Mombo wilayani Korogwe Mei 11, 2017. Kila mtu alishangazwa na ujasiri huo, wakati kwa kitendo hicho alichofanya kilikuwa kinahatarisha maisha yake. (Picha na Yusuph Mussa).
Mbunge wa Korogwe Vijijini kupitia CCM Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu ameaga Dunia jana Julai 2,2018.

Taarifa zinasema Maji marefu alikuwa amelazwa Dodoma kwa matibabu na June 20 akahamishiwa katika hospitali ya taifa ya muhimbili kabla mauti kumkuta.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na uongozi wa hospitali ya Muhimbili.

Ikumbumkwe kuwa mapema tarehe sita mwezi June mwaka huu Profesa Maji marefu alifiwa na mke wake aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Stephen Hilary Ngonyani amezaliwa mwezi mei mwaka 1956, amekuwa mbunge wa Korogwe vijijini tangu mwaka 2010.

Alizidi kupata umaarufu katika ulimwengu wa siasa.

Katika harakati zake za kutetea wananchi Bungeni, mwaka 2016 Ngonyani alitoa hoja ya kupandisha bei ya petrol na kushusha bei ya sukari ili kuwasaidia zaidi watanzania hasa wa hali ya chini.

Kabla ya hapo Ngonyani alifahamika Zaidi kama profesa Maji marefu ambapo alikuwa ni mganga na mtaalamu wa tiba za asili.

Shughuli zake za uganga zili zungumziwa katika mitandao na hata baadhi ya majarida.

Nchini Kenya Stephen Ngonyani ama profesa Maji marefu, aliwahi kuweka kituo cha kazi zake za tiba Kenya na alifanya kazi kama mganga wa kienyeji.

Alimulikwa mnamo mwaka 2010 baada ya kuhusishwa katika mgogoro wa familia ya aliyekuwa mwana siasa maarufu na tajiri.

Taarifa za mazishi yake bado hazija wekwa wazi, lakini Tayari bunge la Tanzania limetoa Taarifa kuwa wata kaa na familia ili kushiriki katika kuratibu mazishi.Read More

Share.

Comments are closed.