Monday, June 24

Picha : RC SHINYANGA AFUNGA MAFUNZO YA WAKUNGA – HUDUMA ZA DHARURA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO

0Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amefunga mafunzo ya wakunga mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga mkoani Shinyanga yaliyoandaliwa na Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA),Cuso Internation na Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM).


Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Mkunga Okoa Maisha ‘Midwives Save Lives’ unaotekelezwa katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu na yalilenga kuwajengea uwezo wakunga wanaotoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya zahanati na vituo vya afya.

Akizungumza jana Julai 4,2018 akifunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa wiki tano na kukutanisha wakunga 100 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Telack aliwashukuru watekelezaji wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha kuchagua mkoa wa Shinyanga kuwa katika mradi ili kuinua kiwango cha utoaji huduma za afya ya mama na mtoto.

Telack alisema wakunga ni kati ya kundi kubwa la wafanyakazi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto katika kutoa huduma kwa wanawake wakati wa ujauzito,kujifungua na baada ya kujifungua hivyo ni muhimu kwa kila mkunga kuwa na stadi muhimu za ukunga za kuweza kuokoa maisha ya akina mama na watoto na kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika.

“Takwimu zinaonesha kuwa mkoa wetu kwa mwaka 2017 akina mama 73 walipoteza maisha kutokana na matatizo yanayotokana na uzazi,kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka 2018 akina mama 20 wamefariki”,

“Hivi sasa kuna mabadiliko kidogo ukilinganisha na mwaka 2017 kwa kipindi hicho kwani Januari hadi Juni 2017 akina mama 26 walifariki,hali hii bado hairidhishi hivyo sisi sote tunatakiwa kuongeza juhudi za kutokomeza kabisa vifo hivi”alieleza Telack.

Alizitaja sababu zilizochangia kutokea kwa vifo hivyo mwaka 2017 kuwa ni kutoka damu nyingi kabla na baada ya kujifungua vifo 25,kifafa cha mimba vifo 10,maambukizi vifo 10,kupasuka kizazi vifo 7,upungufu wa damu vifo 5 na sababu zingine vifo 16.

Alisema vifo vya akina mama na watoto vitazuilika kwa kiasi kikubwa kama wakunga wakiwezeshwa  vizuri katika kutoa huduma kwani takwimu zinaonesha kuwa wakunga wakifundishwa vizuri na kufikia kiwango cha kimataifa wanaweza kutoa huduma kwa asilimia 87 ya huduma zote anazohitaji mama mjamzito na mtoto mchanga.
“Wakunga tumieni pia uzoefu wenu kuhudumia akina mama na watoto,naomba mjue kuwa taaluma mliyonayo mko wachache,itendeeni haki,tunataka kila mama anayebeba mimba azae mtoto aliye hai na hatuna sababu ya kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa uzembe wa mkunga”,aliongeza Telack.
Aidha aliishukuru serikali ya Canada kupitia Global Affairs Canada kwa kufadhili mradi wa Mkunga Okoa Maisha na kuwataka wakunga kutekeleza majukumu yao kwa weledi,umakini ,uzalendo na upendo katika kuwahudumia akina mama na watoto.

Awali akizungumza, Mratibu wa  mradi wa Mkunga Okoa Maisha nchini Tanzania, Martha Rimoy alisema mafunzo hayo ya wiki tano yalilenga kuwapa stadi muhimu za kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga mara inapotokea dharura.

“Katika wiki hizi tano za mafunzo,tumekutana na wakunga 100 hivyo kufanya idadi ya wakunga waliopatiwa mafunzo kuwa 220 baada ya kuwapa mafunzo wakunga 120 mwaka 2017”,alisema.

Naye Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari alisema Mradi wa Mkunga Okoa Maisha unatekelezwa katika nchi nne ambazo ni Ethiopia,Benin,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania,na kwamba kwa Tanzania mradi unatekelezwa katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Aidha aliiomba serikali kuongeza ajira za wakunga kwani ni wachache ukilinganisha na mahitaji yanayotakiwa lakini pia kuhakikisha wakunga wanajengewa nyumba karibu na vituo vya kutolea huduma.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM,Deborah Bonser alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo TAMA katika kuhakikisha kuwa wakunga wanafanya kazi katika mazingira bora.
Hata hivyo, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) Agnes Mtawa aliwataka wakunga kuzingatia maadili ya kazi na kusisitiza kuwa baraza hilo halitasita kumnyang’anya leseni mkunga atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama – Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifunga mafunzo ya Wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga. Pichani ni wakunga 20,waliowakilisha wakunga 100 waliopatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha wiki tano  
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwasisitiza wakunga kufanya kazi kwa weledi,umakini na upendo kwa akina mama na watoto
Wakunga wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Said Yasin,kulia ni Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari.
Mratibu wa  mradi wa Mkunga Okoa Maisha nchini Tanzania, Martha Rimoy akielezea malengo ya mafunzo kwa wakunga 100 waliyoyatoa kwa muda wa wiki 5.
 Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Deborah Bonser akizungumza wakati mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
 Mwakilishi wa Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Deborah Bonser akiiomba serikali kuendelea kushirikiana na wakunga ili kumaliza changamoto ya vifo na mtoto.
Wakunga wakiwa ukumbini
Meza kuu
 Mkunga kutoka Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Patrice Latka akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Mkunga kutoka Chama Cha Wakunga wa Canada (CAM, Jasmin Tecson akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) Agnes Mtawa akiwataka wakunga kuzingatia maadili ya kazi yao.
Mkurugenzi wa Shirika la Cuso International Romanus Mtung’e akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Zoezi la kufunga mafunzo likiendelea
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akiiomba serikali kuendelea kushirikiana na chama hicho katika kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinamalizika mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama Said Yasin akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akizungumza wakati  mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akifunga  mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga.
Mkunga Innocent Rwiza akisoma risala ya washiriki  wa mafunzo hayo
Wakunga wakifuatilia matukio ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi mkunga cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga yaliyofanyika katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimkabidhi mkunga cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wakunga 100 mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma za dharura kwa wajawazito,wazazi na watoto wachanga
Zoezi la kukabidhi vyeti likiendelea
Mkunga akishikana mkono na Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na washiriki  wa mafunzo hayo
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na washiriki  wa mafunzo hayo.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blogRead More

Share.

Comments are closed.