Monday, June 17

JINSI LUGOLA ALIVYOMTIMUA KWENYE KIKAO KAMISHNA WA MAGEREZA

0


 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukiza kikaoni, Kamishna wa Magereza, Juma Malewa kwa kosa la kuchelewa.Lugola amefanya hayo leo, Julai 6 wakati wa kikao cha kimkakati cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo.


Lugola aliagiza mlango kufungwa saa 5 kamili wakati kikao hicho kinaanza. Lakini saa 5:1 Dk Malewa aliingia na hapo hapo Lugola alimwambia atoke nje.


“Nani anayefunguliwa mlango wakati nimesema saa 5 kamili asifunguliwe mtu kuingia kwenye kikao changu isipokuwa mwandishi wa habari?” amesema Lugola


Dk Malewa akajibu: “Ni Mimi hapa, samahani sana.”


Lugola: “hakuna cha samahani hapa.”


Dk Malewa: “Mheshimiwa nimeshafika hapa.”


Lugola: “Hapana hapana rudi nje, nikisema saa 5 ni saa 5 kwa hiyo am very sory (samahani sana).”


Akaongeza: “Wote mliochelewa naomba mtoke nje nawaheshimu sana, tena wengi ni maofisa wakubwa wa magereza lazima tuwe na jeshi lenye nidhamu. Naomba uende nje nakuheshimu sana.”


Hata hivyo baada ya kuzungumza na wanahabari Dk Malewa na maofisa wengine waliruhisiwa kuingia ndani ya kikoa hicho.


Na Bakari Kiango, MwananchiRead More

Share.

Comments are closed.