Monday, August 19

TAIFA STARS YATANDIKWA GOLI 4-1 NA ALGERIA

0Mechi ya kirafiki iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kati ya Algeria dhidi ya Tanzania imemalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Mechi hiyo imepigwa usiku huu katika Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida nchini Algeria.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52′).

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.

Matokeo hayo yanaleta taswira mbovu kwa Tanzania haswa kuelekea kupanda kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki, dhidi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018.Read More

Share.

Comments are closed.