Saturday, August 24

MABAO YA BOCCO, KAGERE YAMPAGAWISHA MO DEWJI SEVILLA WAKIICHAPA SIMBA

0Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ameshindwa kujizuia kwa kushangilia kwa nguvu wakati vijana wake wakichapwa mabao 4-5 na Sevilla kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mo Dewji alishindwa kujizuia ni baada ya kufungwa bao la tatu na John Bocco aliyepokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.

Mo Dewji aliyekuwa ameketi karibu na Mkurungezi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Abbas Tarimba alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka baada ya Simba kupata bao la tatu.

Mo Dewji alikuwa amesimama huku akirukaruka na kumpa mkono wa pongezi Tarimba.

Baada hapo Mo Dewji alikaa chini huku akionekana bado kuwa na furaha akiwapa mkono wa pongezi waliokuwa karibu yake.

Mo Dewji hakushangilia bao hilo peke yake kwa upande wa viongozi waliokuwa jukwaa Kuu ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Magori, Mwenyekiti Swedy Mkwabi.

Na Thobias Sebastian

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

Leave A Reply