Thursday, August 22

VIGOGO SABA CHADEMA WAIBWAGA SERIKALI KORTINI BAADA YA KUSHINDWA KUTHIBITISHA MASHTAKA

0


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Februai 28, 2018 imewaachia huru wanachama 7 wa Chadema, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mashahidi upande wa mashtaka kutoa ushahidi hafifu usio na nguvu kisheria ya kuwatia hatiani washtakiwa hao.

Wafuasi hao saba wa Chadema wakiongozwa na Sunday Urio, walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kuzuia askari polisi kutimiza majukumu yao, ambapo ilidaiwa waliwapiga mawe maeneo ya Ubungo Riverside .Read More

Share.

About Author

Comments are closed.