Tuesday, August 20

TRUMP AISHUKIA FBI KWA KUCHELEWESHA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA WANAFUNZI 17

0


Rais wa Marekani Donald Trump, ameirushia cheche za maneno shirika la upelelezi nchini humo- FBI, kwa kukosa kupata vidokezi muhimu vya mapema, kuhusiana na shambulio la Jumatano huko Florida, wakati mtu mwenye silaha alipowashambulia wanafunzi wa shule na kuwauwa watu 17.

Amesema kuwa FBI inapoteza muda mwingi kujaribu kubaini kuwa timu yake ya Kampeini ya Urais ilishirikiana na Urusi kuiba kura mwaka 2016 badala ya kutoa uilinzi kwa wamarekani.

Katika mtandao wake wa Tweeter, Bwana Trump, ameandika kuwa FBI inafaa kuzingatia kazi yake muhimu, huku akiongeza kusema kuwa, ni huzuni kubwa na ni jambo lisilokubalika kwamba, dalili ya uwezekani wa kutokea mashambulizi, haikutambuliwa mapema.

Awali Maelfu ya watu huko Florida, wakiwemo manusura wa kisa hicho cha Jumatano walijumuika pamoja katika mkutano mkubwa, wakitoa wito wa kuwepo kwa sheria ya udhibiti silaha nchini Marekani.

Aidha Bwana Trump amelaani kitendo hicho kiovu kilichotekelezwa na mvulana Nikolas CruzRead More

Share.

About Author

Comments are closed.