Tuesday, August 20

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA AKWILINA

0


Serikali imesema itagharamia shughuli za mazishi ya aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyefariki dunia siku ya Ijumaa ya Februari 16 mwaka huu baada ya kupigwa risasi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joice Ndalichako wakati akizungumza na wanahabari.

“Msiba mkubwa ambao wizara yangu imepata wa mwanafunzi wa NIT, serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma mwaka wa kwanza NIT, kimetokea wakati wa kudhibiti maandamano katika wilaya ya mkwajuni wilaya ya kinondoni, napenda kuchukua nafasi hii kutoa pole kwa ndugu na familia ndugu, jamaa na marafiki wa Akwilina,” amesema.

Prof. Ndalichako amesema serikali imepata pigo sababu inagharamia wanafunzi kwa kuwapa mikopo, na kwamba marehemu Akwilina alikuwa miongoni mwa wanafunzi walionufaika na mikopo, pia alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa kike aliyejipambanua kuijua thamani ya elimu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.