Sunday, August 25

Mbowe na wenzie watano CHADEMA kula Pasaka Mahabusu – Mtembezi

0


DHAMANA ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na viongozui wenzake watano imeshindikana kutolewa kutokana na madai ya kuwa gari za magereza lililokuwa liwalete mahakamani kuwa mbovu.

Uamuzi wa dhamana hiyo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri aliyesema washtakiwa wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh milioni 20, kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao wa vijiji au mtaa na kuwa, nakala za vitambulisho vyao na kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kila Alhamisi kisha kusema asiyeridhika na uamuzi huo ana haki ya kukata rufaa.

Dhamana hiyo imeshindikana kutokana na watuhumiwa kutokuwepo mahakamani hapo hivyo kushindwa kusaini hati za dhamana zao na kushindwa kutimiza masharti hayo ambapo wangekuwepo, dhamana yao ilikuwa Iko wazi.

Lakini pia baada ya kutolewa dhamana wakili wa serikali aliwasikisha notice ya kupinga dhamana hiyo na upande wa utetezi ukatoa hoja zake za kukataa notice hiyo ambapo baada ya kusikikiza hoja za pande zote, hakimu Mashauri akapinga notice hiyo na kuitaka Jamhuri kama inapinga dhamana hiyo iwasilishe notice baada ya watuhumiwa kusaini hati zao za dhamana.

Mahakama imeamua Mbowe na wenzake wafikishwe mahakamani hapo Jumanne, Machi 3, mwaka huu kutimiza masharti ya dhamana yao ili waachiwe.

The post Mbowe na wenzie watano CHADEMA kula Pasaka Mahabusu appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.