Sunday, August 18

CUF yaitaka Serikali kurejesha misingi ya Taifa – Mtembezi

0


Chama cha CUF kimeitaka serikali, wananchi na wadau mbalimbali kutengeneza mikakati itakayosaidia kulirejesha Taifa katika misingi yake, ili lisiangamie.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Taifa, Julius Mtatiro amesema ipo haja serikali na wananchi kwa ujumla kushirikiana katika hilo ili kutoliingiza taifa katika maangamizo.

Mtatiro alidai kuwa, kuna baadhi ya matukio ikiwemo ya watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha na mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana, pamoja na mashambulizi dhidi ya demokrasia, yaliyotokea siku za hivi karibuni hapa nchini ambayo yameitia doa Taifa, huku akitoa wito kwa serikali kukomesha matukio hayo.

“Jukumu kubwa la serikali ni kulinda haki ya msingi na ya kikatiba ya kuishi. Kuna matukio ya mauaji yalitokea kuna baadhi ya viongozi wa CCM, Chadema na polisi waliuawa. CUF ilitoka hadharani na ikaiomba serikali idhibiti matukio hayo. hadi sasa polisi haijatoka hadharani kuwaeleza watanzania nani aliyeongoza matukio hayo,” alisema.

Alisema iwapo matukio hayo hayatakomeshwa, yanaweza yakajenga chuki na visasi na manung’uniko miongoni mwa jamii.

The post CUF yaitaka Serikali kurejesha misingi ya Taifa appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.