Tuesday, August 20

Mhhh Zari hataki kusikia kuhusu Diamond wala michepuko yake

0


Drama kati ya Zari The Boss Lady na Diamond Platnumz bado zipo pale tena katika kiwango cha juu.


Safari hii Zari amewajia juu wale ambao wanamfuata mtandaoni na kumuuliza kuhusu kuachana kwake na Diamond. Zari akiwa Insta Live ameonyesha kuchukizwa na hilo.
Zari amesikika akisema hii nafasi, hili jukwaa ni kusuhu Zari pekee, sio Diamond, sio mama yake wala michepuke yake na kuongeza maneno makali kidogo, kisha kurudia tena hapa ni kuhusiana na Zari tu.
Utakumbuka Jumatano ya wiki iliyopita katika siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Zari The Boss Lady alitangaza rasmi kuachana na Diamond kutokana na kuchoshwa na habari za kusalitiwa ambazo husikika kila siku katika vyombo vya habari. Katika mahusiano yao Diamond na Zari wamefanikiwa kupata watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’.

Read More

Share.

About Author

Comments are closed.