Thursday, August 22

ZRB yawanoa wanahabari Z’bar

0


 

Mohamed Khamis

Unguja.Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imesema itahakikisha inasimamia vyema Suala la  ulipaji wa kodi ili kuunga mkono utekelezaji wa Mpango wa maendeleo Endelevu (SDGs) katika kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Meneja wa kitengo cha Mahusiano na Huduma ZRB Shaaban Yahya amesema mara baad aya kumalizika kwa mafunzo ya siku ya waandishi wa ahabri ofisini kwao Mazizini mjini hapa.

Alisema ili dhana ya maendeleo iweze kufanikiwa  kwa haraka zaidi haraka ni vyema kila taasisi ikatimiza wajibu wake katika kusimamia majukumu yao.

Alisema  ZRB itaendeleza azma yake ya kuimarisha upatikanaji wa mapato kwa wakati pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokwepa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia malengo ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu kwa wananchi.

Hata hivyo aliwataka wananchi kulipaa kodi kwa mujibu wa sheria hususan kwa wafanya Biashara ili kuuweza mpango huo kutekelezwaa kwa wakati.

Awali akiwasilisha mada juu ya Wajibu wa Waandishi wa Habari katika Kodi Afisa uhusiano wa (ZRB )Makame Khamis Muhammed amesema suala la ulipaji kodi linahitaji mashirikiano ya wananchi wote na sio ZRB peke yao.

Alisema  ni vyema kwa Waandishi wa Habari kutumia vyema taaluma zao katika kuwahimiza wananchi umuhimu wa kulipa kodi ili kuimarisha upatikanaji wa mapato ya Nchi.

Makame amesema Waandishi wa Habari watakapo kuwa msatari wa mbele juu Kuwaelimisha wananchi wataweza kuisadia serikali pamoja na wananchi kunufaika na Vyanzo vya Mapato zilivyopo katika kurahisisha upatikaji WA huduma za jamii.

Akitowa neno la shukurani kwa niabaa ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo Afisa habari kutoka Habari maelezo Faki Mjaka ameahidi kuyafanyia kazi Mafunzo hayo ili mwanachi waweze kulipa kodi bila ya shuruti.

Hata hivyo ametowa wito kwa taasisi nyengine kuwa na utaratibu wa kutoa elimu juu ya Mapango wa Maendeleo endelevu ili wananchi waweze kunufaika na haki zao za msingi.

Mafunzo hayo ya siku mojaa kwa waandishi wa Habari juu ya Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) katika ulipaji kodi yameandaliwa na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

 

Share.

About Author

Leave A Reply