Monday, August 19

Waziri Mwakyembe awashangaa wabunge wanaohoji alipo Azory Gwanda

0


Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameshangazwa na wabunge wanaohoji kutoweka kwa mazingira ya kutatanisha kwa mwandishi wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) mkoani Pwani, Azory Gwanda.

Alisema mwandishi huyo aliyetekwa na watu wasiojulikana Novemba 21, 2017, alipotea  katika mazingira ambayo Watanzania wengi wamekua wakipotea.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 23, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2019/2020.

Alieleza kuwa eneo ambalo alipotea mwandishi huyo waliwahi kupotea pia watanzania wengi sana kwa kipindi hicho na hadi leo hii hakuna alieoneoana hivyo anashangazwa kwanini wengine hawaulizwi au wabunge hao kuhoji.

”Halafu inaulizwa Serikali ambayo imeshughulikiwa kiasi kikubwa na maofisa wa Serikali wengi wamekufa pale, najua mnawalisha wazungu na wafadhili matango pori, hatujakosa chochote acha tushushwe madaraja, sisi tunaheshimu uhuru wetu kwanza.”aliongezea.

Kwa mujibu wa mkewe Azory, Anna Pinoni (35), siku hiyo asubuhi watu wanne wakiwa katika gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe, walifika katikati ya mji wa Kibiti, sehemu ambayo Azory hupatikana mara kwa mara, na kumchukua.
Watu hao walimpeleka hadi shambani ambako mkewe alikuwa akilima na akamuaga kuwa anaenda kazini, lakini hajarudi hadi leo.

Share.

About Author

Leave A Reply