Sunday, August 25

Waziri Lugola apinga ripoti ya CAG dhidi ya jeshi la Polisi

0


Na mwandishi wetu Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amevunja ukimya leo na kusema  taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa Jeshi la Polisi lililipa Sh16.6bilioni bila kuwepo kwa uhahidi wa uagizaji na upokaji wa sare zake hazina ukweli na ni za uongo.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 25, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2019/2020 na kubainisha kuwa ikiwa itabainika jambo hilo ni ukweli yupo radhi kuacha uwaziri.

” Haiwezekani sare zinazodaiwa kuwa hewa mimi Waziri ambaye nimekwenda katika makontena na maghala ya Jeshi la Polisi na kukuta sare nyingi zilizoletwa harafu CAG anapeleka taarifa kwa Rais kwamba hakuna sare.”

Hat“Nanyanyua mikono juu ikifika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa najivua nguo,kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama tukiwa tumeambatana na maofisa wa CAG twende stoo akaone makontena zaidi ya 15 yenye futi 40,” amesema Lugola.

Alisisitiza Kama itaendelea kuwa na mtu anayefanya ukaguzi na kusema uongo hwenda mambo mengi yakaribika na kutaka aogopewe kabisa.

Katika ripoti yake CAG alibainisha ukaguzi wa ununuzi wa sare za askari umebaini jeshi hilo lilipa Sh16.66 bilioni zililipwa bila kuwapo na ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare hizo za polisi wa Boharia Mkuu wa Polisi.

Share.

About Author

Leave A Reply