Friday, August 23

Wavuvi haramu 11 wakamatwa Kiwengwa Z’bar

0


Maafisa wa kikosa cha kuzuia magendo Zanzibar(KMKM) wamefanikiwa kuwakamata wavuvi 11 wakiendesha shughuli zao za uvuvi haramu katika bahari ya kiwengwa mkoa wa kaskazini Unguja.

Zoezi la kukamatwa kwa wavuvi hao limekuja  baada ya msako maalumu wenye lengo la kumaliza matendo hayo ambayo yanaonekana kuwa hatarishi kwa viumbe hai baharini.

Awali akizungimzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya kaskazini B Unguja Rajab Ali Rajab amesema vita dhidi ya uvuvi haramu inaweza kufanikiwa iwapo waliopewa jukumu la kusimamia sheria watatekeleza wajibu wao katika kusimamia hilo.

Alisema iwapo matendo ya uvuvi haramu hayataonewa muhali pindi wanapobainika  baadhi ya watu wenye kutenda hayo na kisha kuchukuliwa hatua stahiki ni wazi kuwa yatakoma na kubaki historia.

Kauli hio ya mkuu wa wilaya ameitoa katika fukwe za bahari ya kiwengwa baada ya taarifa ya kukamatwa kwa wavuvi wenye kutumia zana haramu za kuvulia.

Hata hivyo alieleza kuwa uongozi wa wilaya yake utaendelea kushirikiana na maafisa wa KMKM ili kuhakikisha wanawakamata wale wote wenye kufanya shughuli za uvuvi haramu katika maeneo hayo.

Aidha mkuu huyo amewatak viongozi wa shehia hizo kuangalia kwa kina sheria za uvuvi ili kuweza kuwadhibiti wananchi wanaofanya shughuli hizo kinyume na sheria.

 

Share.

About Author

Leave A Reply