Friday, August 23

Profesa Lipumba alia na Serikali kuzuia ripoti ya IMF

0


Na mwandishi wetu.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba nae leo amevunja ukimya kwa kile kinachoendelea kujadiliwa na wengi Nchini hapa na kumtaka  Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango kuruhusu kuchapishwa kwa ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayozungumzia hali ya uchumi wa Tanzania ili Watanzania wajue yaliyomo.

Lipumba ambae pia ni mtakamu wa uchumi aliyasema hayo leo jinini Dar es salama wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kuzuia  taarifa hiyo ni sawa na kujipiga risasi kwenye mguu na kwamba wanaozuia wapaswa kutambua kwamba wanaopadwa  kuiona ni sisi wananchi, wabunge na hasa wakati huu wabunge la bajeti ili wajue.

“Ni kwamba hio  ripori Serikali wanayo, IMF wanayo, Marekani wanayo, China wanayo, Ujerumani hata wakizuia wengine wanajua. Waruhusu ichapishwe halafu kama kuna kitu hawakubali waeleze wasichokubali,” alisisitiza.

Akieleza kuhusu  utabiri wa IMF kwa uchumi wa Tanzania ambao alisema unapatikana katika World Economic Outlook iliyomo kwenye tovuti ya shirika hilo, Profesa Lipimba alisema shirika hilo limetabiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania kushuka kutoka asilimia 6.5 mwaka 2018 hadi asilimia 4 mwaka 2019.

Awali alisema  IMF walitabiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 6.5 mwaka 2018 hadi 2023 lakini mwaka 2019 wametabiri utakuwa kwa asilimia 4.5 jambo alilosema ni hatari.

“Tabiri zote mbili ni  tofauti za asilimia 2 ni kubwa mno. Huenda wametoa sababu. Ukiangalia Rwanda wamesema uchumi utakuwa kwa asilimia 8 kwa mwaka 2018-23.

“Ili kuwa wazi na kujadili na hasa wakati huu bunge linakutana jujadili Sera wajadili na hasa kama kuna mahali pa kubadili.”

Alisema athari za kushuka huko kwa uchumi zimeanza kuonekana ambapo licha ya makadirio makubwa ya bajeti ya maendeleo, lakini fedha hazipelekwi.

Sambamba na hayo pia alisema kumekua  na makadirio makubwa mno ya bajeti, lakini fedha zinazokwenda sizo. Malimbikizo ya malipo, kuna taasisi zinatoa huduma hazilipwi kwa wakati, sasa mzuuguko wa fedha unapungua.

 

Imehaririwa na Mohamed Khamis

Share.

About Author

Leave A Reply