Sunday, August 18

Mkuu wa Wilaya Chakechake ataka mashirikiano zaidi walimu na wazazi kuongeza ufaulu

0


Na Mohamed Khamis

Pemba.Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadidi Rashid amesema bila ya mashirikiano bora baina ya wazazi na walimu kiwango cha ufaulu  kwa wanafunzi hakiwezi kuongezeaka katika wilaya hio.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na walimu na wazee wa shule  ya Ng’ambwa katika kiwanja cha skuli hiyo jana kufuatia mkakati maalumu ulioandaliwa na wazee wa wilaya hio wenye lengo la kuongeza ufaulu shuleni.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni shule nyingi kwneye wilaya hio zimeshidnwa kufanya vizuri kimasomo kutokana na uwepo wa sababu mbali mbali zinazopelekea mazingira hayo.

Akitaja baadhi ya sababu hizo ni pamoja utoro kwa wanafunzi sambamba na kukosa kw amashirikiano kutoka kwa baadhi ya wazazi ambapo alisema tatizo hilo ipo haja ya kushughulikiwa.

‘’Ni lazima tatizo hili liondoke kwenye wilaya yetu na halitaondoka iwapo mashirikiano ya pamoja hatafanyika baina ya wazee na wanafunzi pamoja na walimu wetu’’aliongezea.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya hiyo, Omar Juma Ali, alisema licha ya uwepo wa chanagmoto hizo lakini pia ipo haja ya walimu hao kuwa wazalendo na kujali zaidi kazi yao.

Alisema inasikitisha kuona kiwango cha ufaulu kimeshuka katika wilaya yake ikiweno shule ya Ngambwa amabpo hapo awali shule hio ilikua na historia kubwa ya ufaulu kwa wananfunzi.

Nae Mwalimu Asma Ali Hafidh, alisema dharau ya wanafunzi kwa walimu na matumizi mabaya ya simu wakati wanafunzi wakiwa darasani imekua ikichangia kuleta matokeo mabaya.

Baadhi ya wazazi wakichangia katika mjadala huo pamoja na matatizo mengine yalipopo lakini pia kuna baadhi ya wazazi wanakosa muamkop na maswala ya elimu na kuwafanya watoto wao kutopenda pia  elimu.

Share.

About Author

Leave A Reply