Monday, August 19

Serikali Yasema Haijaizuia IMF Kuchapisha Hali ya Uchumi wa Tanzania

0Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, amesema Serikali haijalizuia
Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti ya uchumi wa Tanzania
isipokuwa kinachofanyika ni mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na
shirika hilo kabla ripoti hiyo haijachapishwa. 


Dk.
Mpango ametoa taarifa hiyo bungeni leo Jumanne aprili 23, alipokuwa
akitoa ufafanuzi wa maelezo ya Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka
(Chadema), aliyesema Serikali imelizuia shirika hilo kutoa ripoti ya
uchumi wa Tanzania.
Katika
maelezo yake Mwakajoka alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na  Michezo kwa mwaka wa fedha
2019/20, alisema waandishi wa habari wamejaa hofu ya kuripoti mambo
mbalimbali yakiwamo hali ya uchumi wa Tanzania.
Kutokana na hali hiyo alishauri waandishi wa habari waachwe huru ili waripoti mambo mbalimbali kwa maslahi ya umma.

Share.

About Author

Leave A Reply