Friday, August 23

Mkude: Niko tayari kuivaa Njombe Mji – Mtembezi

0


KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amesema kuwa anaendelea vyema na yuko tayari kuitumikia timu yake katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Njombe Mji FC itakayofanyika Jumanne kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Mapema wiki hii Mkude alipata maumivu katika eneo karibu na enka na kulazimika kutolewa nje ya uwanja, lakini tayari amesharejea kuanza kujifua na wachezaji wenzake.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkude, alisema kuwa anaendelea vyema na amewataka mashabiki wa vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokuwa na wasiwasi wowote juu yake.

“Naendelea vizuri, niko vyema na mechi ya Njombe Mji nikipangwa nitacheza,” alisema kiungo huyo.

Simba inatarajia kwenda kuweka kambi ya muda Iringa na baadaye kuanza safari ya kuelekea Njombe Mji kuikabili timu hiyo ambayo iko katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.

Baada ya mchezo huo, Simba itawafuata Mtibwa Sugar katika mechi nyingine ya ligi itakayofanyika Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

The post Mkude: Niko tayari kuivaa Njombe Mji appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.