Saturday, August 24

Mchango wa kilimo pato la taifa wapungua – Mtembezi

0


MCHANGO wa sekta ya kilimo kwenye Pato la Taifa (GDP), umepungua kutoka asilimia 50 ya miaka 1990 hadi asilimia 26 katika mwaka 2017.

Takwimu hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba wakati akifungua Kongamano la siku tatu la sekta ya kilimo lililofanyika mjini Dodoma.

Dk Tizeba alisema ingawa sekta za kilimo na viwanda zina uwezo wa kukuza uchumi na kutokomeza umaskini, ufanisi wa sekta hii kwa sasa umekuwa nyuma.

“Hii inadhihirika wazi ambapo tunaona kwamba asilimia 59.4 ya kaya nchini bado wanaishi chini ya mstari wa umasikini wa mali, asilimia 34.4 ya watoto chini ya miaka mitano wana udumavu,” amesema.

Amesema, kilimo kina jukumu muhimu katika uchumi wa Tanzania, ambapo utafiti unaonesha kwamba kilimo kimeajiri asilimia 65.5 ya nguvu kazi ya nchi na kinachangia asilimia 25 ya GDP.

Kwa mujibu wa Dk Tizeba, kuna ushahidi kwamba mabadiliko ya miundo yanaanza kuweka mizizi katika uchumi kwenye baadhi ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Kwa mfano, nchini Tanzania, kutokana na mabadiliko ya miundo, ajira kwenye kilimo imepungua kutoka asilimia 80 katika miaka ya 1990 hadi asilimia 65.5 mwaka 2017.

The post Mchango wa kilimo pato la taifa wapungua appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.