Wednesday, August 21

Hizi hapa sababu za Jokate kutumbuliwa UVCCM – Mtembezi

0


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo, Jokate Mwegelo ni maazimio yaliyoridhiwa na Baraza Kuu la Jumuiya hiyo.

Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate, umetangazwa jana na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James mjini Dodoma wakati wa Kufunga Kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo, iliyotanguliwa na semina elekezi huku akisisitiza nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Akizungumzia  suala hilo, Shaka amesema sababu za kutenguliwa kwa Jokate inatokana na uamuzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo iliyokutana kwa dharura leo mchana chini ya Mwenyekiti wake, Kheri na kuazimia kwa pamoja ambapo hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya baraza hilo ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa ni ajenda ya kikao.

“Itoshe tu kusema ni utaratibu wa kawaida ndani ya CCM pamoja na jumuiya zake kufanya mabadiliko ya aina yoyote pale wanapoona inafaa,” amesema shaka kwa kifupi.

Jokate ametumikia nafasi hiyo kwa miezi 11 tangu ateuliwe Aprili 24, mwaka jana.

The post Hizi hapa sababu za Jokate kutumbuliwa UVCCM appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.