Saturday, August 24

Alichokisema Rage kuhusu Simba SC kutwaa taji la ligi kuu msimu huu – Mtembezi

0


MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa hakuna kitu kitakachoizuia timu hiyo kutangaza ubingwa mapema msimu huu.

Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 42, huku Yanga wakiwa na pointi 37, wakiwa wametofautiana pointi tano tu lakini Rage amesisitiza kuwa kama Simba hawatabwete­ka, mapema tu watatangaza ubingwa.

“Simba ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa iwapo haita­bweteka, timu nyingi kwa sasa zina udhamini wa kutosha, hivyo kusababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye ligi, hivyo hawa­paswi kuridhika na matokeo.

“Wachezaji wanatakiwa watam­bue kwa sasa wana jukumu moja tu la kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, timu ambayo ilikuwa ina­tishia kidogo ilikuwa Azam lakini kwa sasa yenyewe haipo vizuri sana, hivyo bado inayo nafasi ya kufanya vizuri.

“Ushindani jinsi ul­ivyo hakuna aliyetege­mea Mbao ingetolewa na Njombe Mji kwenye FA, wachezaji wa Simba wasibweteke hata kidogo, waonyeshe nguvu ya kuweza kufanya vyema kwenye ligi,” alisema Rage.

The post Alichokisema Rage kuhusu Simba SC kutwaa taji la ligi kuu msimu huu appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.