Saturday, August 17

Alichokisema Kocha Pierre Lechantre juu ya kiwango cha Mavugo – Mtembezi

0


Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema anafuatilia kwa karibu kiwango cha mshambuliaji wake Laudit Mavugo na amepanga kumbadilisha.

Kauli hiyo ya Lechantre inakuja kufuatia kiwango cha mshambuliaji huyo kuporomoka katika siku za karibuni.

Mfaransa Lechantre alisema Mavugo hatakiwi kukatishwa tamaa na mara watakaporudi safari ya Djibouti atakutana na mshambuliaji huyo na kuweka naye mkakati.

Alisema Simba bado inahitaji huduma ya Mavugo aliye katika ubora ambapo amepanga kumbidilisha na kuwa katika ubora walionao washambuliaji wengine nahodha John Bocco na Emmanuel Okwi.

Aidha aliongeza kwamba Mavugo amekuwa akifanya vyema katika mazoezi ya timu hiyo, lakini anapokuwa uwanjani katika mechi hali ya kujiamini na kupambana hupungua tatizo ambalo atajaribu kulifanyia kazi.

“Hapana, hatutakiwi kukata tamaa Laudit bado ni mshambuliaji mzuri kuna mapungufu madogo yanamtatiza nafikiri kama makocha bado tunanafasi ya kulifanyia kazi hilo,”alisema Lechantre.

The post Alichokisema Kocha Pierre Lechantre juu ya kiwango cha Mavugo appeared first on Mtembezi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.