Sunday, August 18

MULTICHOICE YAZINDUA KITUO CHA KISASA MLIMANI CITY

0


KATIKA kuimarisha na kuboresha zaidi huduma zake na pia kuzifikisha karibu zaidi na wateja, MultiChoice Tanzania imefungua kituo kipya cha kisasa cha Mlimani City jijini Dar es Salaam huku ikitoa ofa kabambe ya ufunguzi ambapo wateja wataweza kuunganishwa na DStv kwa shilingi 69,000 tu, hii ikijumuisha vifaa vyote. 
Pia mteja atapata hduma ya ufundi na kifurushi cha miezi miwili bure! Ofaa hii ni kwa wateja wapya wa kituo hicho na itaendelea hadi tarehe 18 Februari 2018

Kituo hicho ambacho kina mandhari nzuri, vifaa vya kisasa na wafanyakazi waliobobea, kitakuwa kinatoa huduma zote kwa wateja wa DStv, kuanzia mauzo ya vifaa, ufundi, huduma za malipo na huduma kwa wateja kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande, amesema kua ufunguzi wa kituo hiki cha kisasa ni sehemu ya mkakati mkubwa wa MultiChoice Tanzania wa kuboresha na kusogeza zaidi huduma zake kwa wateja wake ambao wanaongezeka kwa kasi.

Amesema mkakati huu ni kwa nchi nzima na siku chache zijazo watafungua kituo kingine kama hicho jijini Mwanza na kisha Dodoma, na Mbeya na pia kituo cha Arusha kitaboreshwa na kuwa cha kisasa.

“Tuna mkakati mkubwa wa kuboresha zaidi na kuwasogezea wateja wetu huduma zetu karibu na walipo na kwa mkakati huu tunafungua vituo maalum vya kisasa kabisa vyenye uwezo wa kutoa huduma zote za DStv, kuanzia mauzo ya vifaa, malipo, huduma za kiufundi, mafunzo na ushauri na pia huduma kwa wateja kwa ujumla” alisema Maharage na kuongeza kuwa ndani ya mwaka huu, mbali na vituo hivyo katika miji mikubwa, pia watafungua vituo katika miji midogo na viunga vya miji mbalimbali. “Hatutaki mteja aende mbali ikiwa king’amuzi chake kina hitilafu ya kiufundi, au ikiwa anataka kufanya malipo, au hata kama anataka kufahamu zaidi kuhusu huduma zetu. Tunataka huduma hizi ziwe karibu nao hivyo tumeamua kufungua vituo hivi kila kona ili wateja wetu wapate huduma bora karibu nao.

Ameviataja viunga ambavyo vipo katika mpango wa kuwa na vituo vya huduma kwa wateja ikiwemo Mbagala, Tabata, Oysterbay, Mbezi Beach, Geita, Himo, Tunduma Kigoma, Bukoba na maeneo mengine.

Amesema mkakati huo hauishii tu katika kuweka vituo karibu na wateja, bali pia kuimarisha kituo kikuu cha huduma kwa wateja ikiwemo kuongeza wafanyakazi na pia kuanza kutoa huduma kwa saa 24. “Kwa hivi sasa wateja wetu wanapata huduma kwa saa 24, kwani baada ya muda wa kawaida wa kupokea simu kumalizika saa nne usiku, sasa tunatoa huduma ambao wanapatikana mtandaoni kwa njia ya facebook saa 24.
 
Amesema tangu kuanza kwake miaka 20 iliyopita, MultiChoice Tanzania imekuwa muhimili mkubwa katika ukuaji wa sekta ya Habari na burudani hapa nchini na katika miaka ya hivi karibuni imeweka msukumo mkubwa katika maudhui ya kitanzania hususan baada ya kuanzishwa kwa chaneli maalum ya Maisha Magic Bongo ambayo imesheheni maudhui ya kitanzania.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.