Sunday, August 25

MKURUGENZI TBC ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI ILIYOUWA WAWILI KASULU

0


 Gari la Mkurugenzi wa TBC, Dk Ayoub Rioba likiwa limepinduka baada ya lupata ajali.
Na Rhoda Ezekiel, FK Blog Kigoma.
WATU wawili wamepoteza maisha huku Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji TBC Ayub Rioba amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Kibondo kwenda Kigoma mjini kupata ajali katika  Kijiji cha Mgombe Kata ya Nyakitonto Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza leo mara baada ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Kigoma, Martini Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majinia ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto na Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto ambae hali yake ni mbaya na anendelea naatibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Alisema katika ajali hiyo Waliokuwemo kwenye gari mbali na Dk Rioba ni Mkurugenzi wa Vipindi TBC na Meneja wa Vipindi Kanda ya Magharibi Zabron Mafuru na Dereva aliefahamika kwa jina la Abubakari ambapo wao wamepata majeraha madogo madogo na wamepatiwa matibabu na wanaemdelea vizuri.

Kamanda Otieno alisema Chanzo cha ajari hiyo ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo na kuwaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.