Monday, March 25

BANC ABC YAWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA WANANCHI.

0


Meneja wa Banc ABC tawi la Arusha, Magabe Nyambuche akizungumza jijini Arusha leo.

Na Mwandishi wetu, Arusha.
Banc ABC nchini imeendelea na juhudi za kuwekeza
kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kusaidia jamii kupata
bima  za afya ili kuharakisha maendeleo ya
jamii nchini Tanzania.
Akizungumza jijini Arusha leo Meneja wa Banc ABC
tawi la Arusha, Magabe Nyambuche amesema kwa mwaka huu 2019 wamejipanga kutoa
mikopo kwa vikundi maalum vikiwemo vikoba na  Saccos.
Vikundi mbalimbali vimekuwa vikipewa mafunzo na
maafisa ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za
uzalishaji mali na kujinyanyua kiuchumi na taifa kwa ujumla.
Nyambuche amesema Banc ABC imekuwa karibu na
jamii hata kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali kupitia ubunifu wa kutoa
huduma za kifedha kwa njia ya mtandao  na
kuiwezesha benki hiyo kutwaa tuzo ya Ubunifu.
“Tunamawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa
wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo,” alisema Nyambuche.
Banc ABC imedhamini mkutano mkuu  wa wadau wamaendeleo  yajamii jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo
ya kusaidia jamii ambayo hunufaika na utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika maeneo
ya vijiji  na mijini.
Pia, Banc ABC imejizatiti katika kuendelea kushirikiana
na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutumia dhana ya uwezeshaji wamikopo
yenye masharti nafuu.


Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply