Saturday, August 17

2 of 433 MKUU WA MKOA KILIMANJARO MH ANNA MGHWIRA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KUKAGUA UTENDAJI WA TANESCO MKOANI KILIMANJARO

0Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka, pembeni ni Mhandisi mkuu wa mkoa Bagabuje Joseph, Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba na Meneja wa Tanesco Himo,  Mohamed Kayanda.

Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yared Ngalaba akifafanua kwa Mkuu wa mkoa, Anna Mghwira mifumo ya usafirishaji umeme mkoani Kilimanjaro.
Kutoka kushoto Mhandisi usafirishaji mkoa wa Kilimanjaro Yaredi Ngalaba, Mhandisi mkuu Bagabuje Joseph, Afisa uhusiano Tanesco Kilimanjaro, Samuel Mandari na Meneja wa Tanesco Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,  Anna Mghwira.
Msimamizi wa kituo cha kupoza umeme cha Kiyungi Joseph Mwisongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa, Anna Mghwira.

KATIKA ZIARA HIYO AMETEMBELEA VITUO VYA KUPOOZA UMEME (SUBSTATIONS) ZA KIYUNGI, TRADE SCHOOL, BOMA MBUZI NA KIA.

Mkuu wa Mkoa Amewataka watumishi wa TANESCO kuendelea Kutekeleza majukumu yao kwa bidii ili kuhakikisha huduma ya umeme inakuwepo muda wote na ameahidi kuwaunga mkono katika ulinzi wa miundombinu ya umeme mkoani hapa.

Nae meneja wa TANESCO Kilimanjaro mhandisi MAHAWA MKAKA amemuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwepo kwa umeme wa kutosha kwa wawekezaji wa viwanda Mkoani Kilimanjaro.

Katika Ziara hiyo Mkuu wa mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na wakuu wa wilaya za Moshi na Hai pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa na Wilaya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.