Sunday, August 25

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa

0Charles James, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kwa wanahabari Meneja program ya vijana na maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt Majaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho hayo yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yana lengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.

Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.

“Mwaka huu ni maadhimisho ya 20 ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania iliyopendekezwa kuelekea 2030 ni Tanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajili ya maendeleo ya vijana.

“Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na mada mabalimbali ikihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi wa Kijana wajibika kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha hata vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.

Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.
Meneja Program Maalum ya vijana kutoka Umoja wa Mataifa, Dk Majaliwa Marwa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo kuhusiana na kongamano la vijana litakalofanyika kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa

Share.

About Author

Leave A Reply