Friday, May 24

Wafanyabiashara Jijini Dodoma Waunga Mkono Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

0


Baadhi ya wafanyabiasha katika Jiji la Dodoma wametoa maoni yao kuhusu katazo la matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni 2019 nakusema kuwa katazo hilo limekuja wakati sahihi.

Akizungumza na mwandishi wetu Katibu Mkuu wa Soko Kuu la Majengo, Jijini Dodoma, Eliamani Mollel amesema kuwa wao kama viongozi wamepokea na kuunga mkono marufuku ya kutotumia na kufanya biashara ya mifuko ya plastiki, Serikali ina nia ya dhati kabisa kukataza hii mifuko kutokana na uharibifu wa mazingira, sisi wenyewe ni mashuhuda tunaona mifuko inaleta uharibifu wa mazingira, kuziba kwa mitaro ya maji na adha zingine nyingi zinazofanana na hizo, kwa hiyo sisi kama viongozi kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji , jiji kwa ujumla tunaunga mkono hili la Wazari Mkuu la kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki.

Akichangia maoni hayo Mfanyabiashara wa Vifungashio vya biadhaa ikiwemo mifuko ya plastiki katika Soko la Majengo Jijini Dodoma, Isack amesema kuwa licha ya mud uliotolewa kuwa mfinyu lakini yupo tayari kuhakikisha ifikapo tarehe 1 Juni 2019 anakuwa amekwisha acha kuuza mifuko ya plastiki baadala yake atakuwa anauza mifuku ambayo inakubalika kwa mujibu wa katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni.

Naye Evarist Korneli Sanzi, Mfanyabiashara wa Soko la Changombe Jijini Dodoma amesema kuwa binafsi amefurahishwa sana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotolewa na Waziri Mkuu kwani mifuko hiyo imekuwa ikiharibu mazingiora na uchafu na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angekuwa amekemea siku nyingi sana kwa sababu imekuwa ni kero, lakini aliposikia tamko la Waziri Mkuu amefurahi sana.

Share.

About Author

Leave A Reply