Saturday, August 24

SHULE YA MSINGI HOLILI YAPEWA MIFUKO YA SARUJI 300 KUFANIKISHA UJENZI WA MADARASA 10, NYUMBA ZA WALIMU

0


Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Godwin Kamando (kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs Milioni 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze (Ward Executive Officer) (watatu kulia) na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.

Meneja Afya, Usalama na Mazingira wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Emmanuel Ntoma (wa pili kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.

Meneja Ugavi wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Livin Masawe (wa pili kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs Milioni 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (wapili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Watatu kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.

Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KAMPUNI ya Tanga Cement (TCPLC), imetoa msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa Shule ya Msingi ya Holili yenye thamani ya Sh.3,388,488 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuimarisha sekta ya elimu.

Makabidhiano ya msaada huo yamefanyika katika kampuni hiyo iliyopo eneo la Pongwe mkoani Tanga ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali Kata ya Holili na maofisa wa kiwanda hicho wameshuhudia makabidhiano hayo.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tanga Cement Godwin Kamando amesema lengo lao ni kusaidia maendeleo ya Kata ya Holili na wameona haja ya kusaidia sekta elimu kwa kutoa mifuko hiyo ya saruji kwa ajili ya Shule ya Msingi Holili.

“Msaada huu wa mifuko ya saruji ambayo tumeitoa katika Kata ya Holili ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Holili na hasa kwa kuitumia kujenga nyumba mbili za walimu, ofisi mbili za shule na ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa 10,”amesema Kamando.

Ameongeza moja ya mkakati wao ni kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii ya Watanzania kwa kusaidia shughuli za maendeleo na msaada huo ni maalumu kwa ajili ya eneo hilo la Holili ambalo wao wamekuwa wakipata sehemu ya malighafi kwa shughuli za uzalishaji wa saruji.

” Malighafi inayopatikana eneo la Holili ni madini aina ya Pozzolana ambayo ni muhimu sana katika kutengeneza moja ya aina ya saruji,”amesema na kuongeza wanaamini msaada huo utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kamando amefafanua pamoja na kusaidia katika shule hiyo, wamekuwa wakisaidia katika shughuli nyingine za kimaendeleo na hasa ya ujenzi wa miundombinu katika afya, elimu na mazingira na hadi sasa ndani ya kata hiyo wameshatoa jumla ya mifuko ya saruji 1150. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Kata wa Holili Fadhili Buzebuze amesema wanashukuru kupata msaada huo wa mifuko ya saruji na kufafanua watahakikisha mifuko hiyo inatumika kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa.

Share.

About Author

Leave A Reply