Thursday, August 22

RUKSA WANANCHI JIJI LA MBEYA KUWASILISHA KERO ZAO MBELE YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI-MWENYEKITI WA CCM MBEYA

0


Na EmanuelMadafa,Mbeya

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini Humphrey Nsomba, amesema ni ruksa wanachi wa jiji la Mbeya kuwasilisha kero zao mbele ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ambaye anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye sikuku za mei mosi zitakazo kitaifa Jijini Mbeya .

 Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujuo wa rais Magufuli jiji la Mbeya, Nsomba amesema kuwa  chama cha mapinduzi Mbeya mjini kimejipanga kikamilifu kumpokea kiongozi huyo mkubwa, kwani ujio wake utakuwa chachu ya maendeleo.

“Tumefurahi sana sisi kama Chama Wilaya ya Mbeya Mjini kuhusu ujio wa Mh Rais Katika Sherehe za Mei Mosi ambazo kitaifa zitafanyika  Jijini Mbeya,kwa Upendo huu ambao ametupa sisi wanambeya   tutajitokeza kwa wingi kwani tunahamu  kubwa ya kumuona na kusikia mambo mazuri kutoka kwake.”Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Mbeya Mjini ,Afrey Msomba..

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kukubali kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Mei mosi ni heshima kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi na Mkoa wa Mbeya kwa Ujumla.

Amesema Rais Magufuli ametoa kiasi cha Shilingi Bil12 kwa ajili ya ujenzi wa barabara sita za Jiji la Mbeya pamoja kutoa Fedha za ujenzi wa Kituo cha Iyunga na Nzovwe hivyo wanakila sababu ya Kumshukuru.

Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti huyo wa Ccm Wilaya ya Mbeya mjini amewataka wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali itikadi ya vyama vyao kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za Meimosi ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini hapa .

Share.

About Author

Leave A Reply