Friday, August 23

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA TCRA KUTOZIFUNGA LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA

0Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS
Dk.John Magufuli amesema mchakato wa kusajili laini za simu kwa
kuunganisha na Kitambulisho cha Taifa(NIDA) usogezwe mbele hadi Desemba
mwaka huu huku akiagiza Watanzania wasiokuwa na vitambulisho vya NIDA
wasihukumiwe kwa laini zao kufungiwa.

Kabla
ya kauli hiyo ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo Aprili 26,2019 akiwa
mkoani Mbeya ,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) walitangaza kuwa
watazima laini za simu ambazo hazitakuwa zimesajiliwa na kuunganishwa na
NIDA kwa kuweka alama ya kidole kigumba ambapo pia walitangaza kuanza
kwa usajili wa laini za simu kuanzia tarehe moja ya mwezi ujao.

Akizungumza
leo akiwa ziarani mkoani Mbeya pamoja na mambo mengine Rais Magufuli
amezungumzia usajili wa laini za simu uliotangazwa na TCRA ambapo
amesema hakuna sababu ya kuwahukumu Watanzania kwa kuzima laini zao za
simu kwa kigezo kwamba hawajasajili laini za simu.

Amesema
ifahamike si kwamba anazuia usajili wa laini kwani ni muhimu na usajili
huo una faida zake na ni nyingi lakini amefafanua Tanzania kuna
Watanzania zaidi ya milioni 50 na wenye vitambulisho vya NIDA hawafiki
milioni 15.

Hivyo amesema
ni vema TCRA waongeze muda wa kusajili laini za simu kwa kwenda
sambamba na utoaji wa vitambulisho vya Taifa. “Watu wasihukumiwe kwa
kutosajili simu kwasababu ya NIDA.Mchakato uende pamoja ili watazania
wasiopata wasihukumiwe,” amesema Rais Magufuli .

 

Amesisitiza
kadri NIDA wanavyotoa vitambulisho ndivyo kasi yake iendane na usajili
wa laini za simu,hivyo wasifungue laini kwa kipindi hiki kwani kufanya
ni sawa na kuwahukumu Watanzania.

Wakati
huo huo Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuanza
kuchunguza upya madai ya mtoto wa miaka minne wa kiume kulawitiwa.Rais
ametoa maagizo hayo baada ya mmoja aliyekuwa katika mkutano wa Rais
kupata nafasi ya kuzungumza mbele take ambapo alitoa malalamiko ya mtoto
wake kulawitia.

Mama
huyo baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza amemwambia Rais Magufuli kuwa
mtoto wake wa kiume amelawitiwa na sasa anajisaidia muda wote na baada
ya kitendo hicho aliamua kwenda kwenye vyombo vya ulinzi na usalama
lakini hadi sasa haana msaada wowote zaidi ya kuzungushwa.

Amesema
kuwa amekwenda kuonana na Kamanda wa Polis Mbeya,Mkuu wa Jeshi la
Polisi ncbini IGP pamoja na Jaji Mkuu lakini anaona anazungushwa
tu,hivyo matumaini yake yamebaki kwa Rais Magufuli ambaye ni Rais wa
wanyonge.

“Rais wangu
naomba msaada wako,nimekwenda kila mahali hadi kwa Jaji Mkuu,nisaidie
mheshimiwa Rais ,nyaraka za note ambako nimekwenda ninazo.Mtoto
aliyelawitiwa ni mwanaume na picha yake ninayo,lakini kwenye makaratasi
wanasema ni mwanamke,” amesema mama huyo wakati anamuleza Rais.

Hata
hivyo Rais alimuuliza kama amekwenda na mtoto huyo mkutano hapo lakini
mama huyo akajibu ameshindwa kwenda naye kwani anajisaidia Mara kwa
mara,hivyo hakuweza kufika naye

Kutokana
na maelezo hayo Rais Magufuli alimhakikishia mama huyo kuwa uchunguzi
utafanyika na haki itatendeka ambapo ameomba nyaraka akabidhiwe
mwanasheria ili kuanza ufuatiliaji.

Pia
Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha mama huyo
hasumbuliwi huku akimpa fedha kwa ajili ya kujikimu na mtoto wake.

Share.

About Author

Leave A Reply