Saturday, August 24

NYONGO ASHUHUDIA JIWE LA ALMASI LA UZITO WA “CT” 512.15 LIKIUZWA KWA BILION 3, 262, 149, 332

0


Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akionyesha jiwe la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 mali ya mchimbaji mdogo bwana Joseph mkazi wa Shinyanga. Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Prof. Mruma na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. 

Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Mruma akimuonyesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo jiwe la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 wakati wa mauzo yake yaliyofanyika katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga. 

Bi. Dorcas Moshi, Mchambuzi na Mthamini wa Madini ya Vito na Almasi kutoka tume ya Madini akiifunga rasmi Almasi ya Josephy Temela mara baada ya kukamilika kwa taratibu za uthaminishaji na kupata ghara halisi huku ikishuhudiwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mwenye suti ya Blue. 

Bw. Joseph Temba mchimbaji mdogo ambae ameuza jiwe lake la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani ya Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 wakati wa mauzo yake yaliyofanyika katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga. 

Na: Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) – Shinyanga 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameshuhudia mchimbaji

mdogo wa madini ya almasi bwana Joseph akijizolea fedha, dola za

kimarekani (USD) milioni 1, 418,510.82 ambazo sawa na Tsh. bilioni 3,

262,149,332.75 kutokana na mauzo ya jiwe moja lenye uzito wa Kareti

(ct)512.15. Shuguli ya mauzo ya Almas hiyo imefanyika leo tarehe

25/05/2019 katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga na kushuhudiwa

pia na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Mruma na vyombo mbalimbali

vya usalama na wawakilishi wa benki ya CRDB Shinyangai. 

Akiongea wakati wa kushuhudia mauzo hayo , Naibu waziri Nyongo

amesema, kutokana na mauzo hayo serikali itapata USD 103,551.29 sawa

na Tsh. milioni 238,136,901.61. Ameongeza na kusisitiza kuwa, adhima ya

serikali ya awamu ya tano ni kuwezesha shuguli za wachimbaji wadogo na

wadau wote wa sekta ya madini kufanyika kwa utaratibu unao eleweka

kwa faida yao na ya serikali. 

“Nimpongeze bwana Joseph ambae anauza almasi yake hapa leo kwenye

soko hili la madini, kila kitu kinakuwa wazi mbele ya serikali, polisi, watu wa

usalama na wawakilishi wa Bank ya CRDB, bila usumbufu wowote, na hiki

ndicho tunachokitaka sisi kama serikali, wachimbaji wote kufuata utaratibu

tuliouweka.

Niwaombe wachimbaji kwa mara nyingine, acheni kuuza madini

mchochoroni haita wasaidia zaidi ni kuhatarisha usalama wenu, na pengine

hata kupunjwa kutokana na kuto kujua thamani halisi na bei ya madini yenu

igeni mfano wa bwana Joseph, na niwaambie ukweli ukikamatwa unauza

madini nje ya soko madini hayo yanataifishwa, hivyo utakuwa umekula

hasara na utachukuliwa hatua za kisheria.” amesema Nyongo. 

Kwa upande wake Afisa msaminishaji madini kutoka tume ya Madini Bi.

Dorcas Moshi, Mchambuzi na Mthamini wa Madini ya Vito na Almasi

kutoka tume ya Madini aliekuwa anafanya shuguli nzima ya uthaminishaji

wa Almasi hiyo, amefafanua kuwa fedha iliyopata serikali, Milioni

238,136,901.61 inajumuisha Mrabaha wa USD 85,110.65 sawa na Tsh.

Milioni 195,728,959.97, Ada ya ukaguzi ni USD 14,185.11 sawa na Tshs.

32, 621, 493, .33 na Mrabaha wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ilikotokea Almasi hiyo (Service Levy) ni USD 4,255.53 sawa na Tsh. 9,

786,448. 

Kwa upande wake Kamishina wa Madini prof. Mruma amewasisitiza

wachimbaji wadogo kuzingatia sheria na taratibu hususani kuchimba

kihalali kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni za uchimbaji na kulipa tozo

zote za serikali kwani serikali ipo kwa ajili yao hivyo hawana sababu ya

kuikwepa. 

Kwa upande wake bwana Joseph mmiliki wa almasi hiyo, ameishukuru

Wizara ya madini na Tume ya madini kwa utaratibu waliouweka katika

kutoa muongozo na usimamizi wa namna ya mauzo ya madini

unavyotakiwa kufanyika, ulinzi wa madini yao pindi wanapoyapata na

ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wenzake kuwa hakuna sababu ya

kuyakimbia masoko yaliyoanzishwa na serikali kwani yanafaida nyingi

ikiwemo usalama, ulinzi, uwazi na utambuzi wa thamani halisi ya madini

kitu ambacho nadra sana kwenye masoko yasiyo rasmi.

Share.

About Author

Leave A Reply