Tuesday, August 20

Naibu Waziri Shonza awataka Watanzania Kuandaa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya Muziki kuanzia ngazi ya Wilaya Mpaka Mkoa

0


Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kulia) akiwasili
katika viwanja vya   Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) jana na
kupokewa na vijana wanaoshiriki mashindano  ya Kabati Star Search ambapo
mashindano hayo yanafanyika hapo, watatu kushoto ni  Ritha Kabati
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa ambaye ndiye mwandaaji wa
mashindano hayo.

PIX 4 B

Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (wapili
kushoto)akisalimiana na mchekeshaji maarufu Baraka Mwakipesile
anayeigiza kama Rais Magufuli ambapo kwa sasa anajulikana  kama Baraka
Magufuli mara baada ya uzinduzi wa mashindano ya Kabati Star Search
yaliyofanyika jana Mkoani Iringa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Mufundi Bw.Netho Ndilito.

PIX 4PIX 5

Mmoja ya washiriki wa mashindano
ya  Kabati Star Search Yahya Hamadi  kutoka Kata ya Mwangata  Mkoani
 Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa Msanii Young Killer
katika mashindano hayo yaliyofanyika jana ambapo yalizinduliwa na Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
(hayupo pichani).

PIX 6

Mmoja ya washiriki wa mashindano
ya  Kabati Star Search Sophia Kalinga kutoka Kata ya Gangilonga  Mkoani 
Iringa  akionyesha uwezo wake kwa kuimba  wimbo wa You Raise Me Up 
kutoka kwa msanii Josh Groban katika mashindano hayo yaliyofanyika jana
Mkoani hapo.

PIX 7

Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (watatu kushoto ) akiwa
katika picha ya pamoja na Majaji wa Shindano la Kabati Star Search mara
baada ya uzinduzi wa shindano hilo lililofanyika jana  Mkoani  Iringa,
wapili kushoto ni muandaaji wa shindano hilo Ritha Kabati Mbunge wa Viti
Maalum (CCM) Mkoa wa Iringa .

PIX 8

Msanii wa Mkoa wa Iringa Ezra
Msiliova maarufu kama Eze Nice akiimba  kwa hisia wimbo  wa kuisifia
Tanzania mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa uzinduzi wa Shindano la Kabati Star
Search lilofanyika jana Mkoani Iringa.

………………………………………………………………………………

Na Anitha Jonas- Iringa

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ameto wito  kwa  wadau mbalimbali
nchini kujitokeza kuandaa Mashindano ya kusaka vipaji vya Muziki kwa
vijana kwa kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya.

Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo
jana Mkoani Iringa alipokuwa akizindua Tamasha la Ritha Kabati Star
Search lililolenga kusaka  vipaji vya vijana wanaojua kuimba muziki na
tamasha hilo limekusanya vijana zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali ya
wa Mkoa wa Iringa.

“Ninapenda kumpongeza Mhe.Ritha
Kabati  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kwa kuandaa Tamasha lenye
tija kwa taifa kama hili, pia ninaomba wadau mbalimbali wenye uwezo
kuandaa matamasha kama haya kwa kuanzia ngazi za mbalimbali ndani ya
mikoa na wilaya zetu kwa ndiko waliko vijana wenye vipaji,  tuwasaidie
kufikia ndoto zao kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika
uzinduzi huo wa Kabati Star Search Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa
Utamaduni wa Mkoa wa Iringa kuandika barua kwa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) ya kuomba wataalamu kuja kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi wa
muziki wa mkoa huo kwa lengo la kuwa ongezea maarifa wasanii hao.

Naye muandaaji wa Tamasha hilo
Mhe.Ritha Kabati alieleza kuwa amekuwa akiwaona  vijana wa mkoa huo na
kuwa wanavipaji  ila wamekuwa wakikosa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao
na ndiyo maana aliamua kuanzisha mashindano hayo ambayo yatawainua
vijana wa mkoa wa Iringa nao kuanza kusikika Kitaifa na Kimataifa kama
wasanii wengine maarufu hapa nchini.

“Katika kuhakikisha mashindano
haya yanaleta mafanikio nilizungumza na mmoja wa walezi  wasanii wa
Muziki  nchini  Bw. Said Fella Maarufu kama Mkubwa Fella kuhusu
kuwasaidia washindi wa mashindano haya na tukakubaliana kuwa mshindi wa
kwanza mpaka watatu  atawachukua na kwenda kuwafunza vizuri kisha
watarekodi  nyimbo zao na pia wataimba na wasanii maarufu hapa nchini na
atahakikisha na hizo nyimbo zao zinapigwa katika vituo vya redio na
televisheni mbalimbali nchini,”alisema Kabati.

Pamoja na hayo Kabati alieleza
kuwa vijana wa Iringa wamesema wanataka nao Mkoa wao uonyesha  kuwa
unavipaji vyenye uwezo mkubwa wakufikia ngazi za Kimataifa kwani
 kupitia mashindano ya mpira wa miguu ya Kabati Challenge Cup vijana
watatu tayari wamechukuliwa na timu za mpira za Afrika Kusini kwa lengo
la kwenda kuchezea timu za vijana na watakuwa wanasomeshwa huko pia .

Halikadhalika na mmoja wa
washiriki wa mashindano hayo  Yahya Hamadi alimshukuru mbunge huyo wa
viti maalum kwa kuandaa mashindano hayo na ameahidi kuwa atajitahidi
kufanya vizuri kwani  anaamini  kupitia jukwaa hilo nae anaweza kuja
kuwa msanii maarufu katika Taifa.

Hata hivyo Naibu Waziri Shonza
aliwasihi majaji wa mashindano hayo kutenda haki katika maamuzi
wanayoyafanya kwani  wao ndiyo wenye dhamana ya  kutoa msanii
atakayetangaza mkoa na taifa kwa ujumla katika ngazi za Kimataifa,ambapo
mmoja  wa majaji hao Bw.Roger Magoha kwa niaba ya wenzake aliahidi
kusimamia hilo.

Share.

About Author

Leave A Reply