Sunday, August 18

MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA YANAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA -WAZIRI WA AFYA

0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu amesema mapambano dhidi ya Malaria yanaonesha mafanikio makubwa
kutokana na kushuka kwa Maambukizi hayo kutoka aslimia 14.5 mwaka 2015
hadi kufikia aslimia 7 mwaka huu.

Waziri
Ummy amesema licha ya kushuka kwa maambukizi hayo lakini bado kuna
mikoa kadhaa ambayo bado maambikizi ya ugonjwa wa Malaria yapo juu na
hivyo kutoa wito kwa wadau kuongeza jitihada katika kuutokomeza kabisa
ugonjwa huo.

Mhe.
Waziri ameitaja mikoa ambayo maambukizi ya ugonjwa Malaria yapo juu
kuwa ni pamoja na Mara, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo
amewataka wananchi kuongeza jitihada katika kupunguza kiwango cha
Ugonjwa huo.

“Licha
ya jitihada zinazofanywa kumaliza ugonjwa huu lakini bado jitihada
zinahitajika zaidi katika kufikia lengo la ZERO MALARIA ifikapo 2030”.
Amesisitiza Mhe. Ummy.

Kuhusiana
na maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Malaria Duniani, Mhe. Ummy
amewataka wananchi wote kushiriki katika kufikia lengo la Zero Malaria
kwa kutomeza mazalia ya Mbu, kutumia vyandarua vilivyowekwa Dawa, kwenda
hospitalini pindi wanapohisi wana viashiria vya Malaria na kumaliza
dozi kama watakavyo elekezwa na watalaamu wa Afya.

“Wito
wangu kwa watanzania wote ni kuhakikisha wanafuata maelekezo ya watoa
huduma za afya pindi wauguapo Malaria na pia kuweka mazingira yao safi
ili kukabiliana na mbu waenezao Ugonjwa wa Malaria” Alisema Mhe. Waziri.

Kauli
mbiu ya maadhimisho ya Malaria kwa Mwaka huu ni ZIRO MALARIA INAANZA NA
MIMI huku maadhimisho ya Siku ya Malaria hapa nchini yanatarajiwa
kufanyika April 25, Mkoani Lindi.

Share.

About Author

Leave A Reply