Sunday, August 18

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAWAHUKUMU RAIA SABA WA SOMALIA KIFUNGO CHA MAISHA GEREZANI

0


 


Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu raia saba wa Somalia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya uharamia wa kuvamia meli na kuipiga risasi.

Washtakiwa hao walihukumiwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Mlyambina baada mahakama kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mlyambina amesema, ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa na wote wametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kufungwa jela maisha.

Washtakiwa waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo hicho ni Mohammed Nuru, Bashir Rooble, Muhsin Haji, Abdulwaidi Abdallahamani, Farahani Abdul, Ally Ally na Omary Mohammed.

Wote walikuwa wanakabiliwa na kosa la uharamia kinyume cha kifungu cha 66(1)(a)((I) na (2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Katika kesi hiyo upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Cecilia Shelly na Wakili wa Serikali, George Barasa huku washtakiwa wakijitetea wenyewe.

Katika hati ya mashtaka imedaiwa, Oktoba 3 mwaka 2011 majira ya saa moja na nusu usiku maeneo ya Bahari ya Hindi, maharamia hao walifanya uvamizi kwenye meli ya Sams All good kwa kuipiga risasi hadi wanajeshi wa majini walipoanza kuipiga boti ndogo aina ya Skiff.

Wanajeshi hao walifanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Pwani na February 29, mwaka huu ikasikilizwa na kutolewa maamuzi.

Wakati wa keai hiyo, washtakiwa waliwakilishwa mahakamani hapo na mawakili, Aloyce Komba, Domicus Mkwera, Rupia Abraham, Omary Msemo, Dennis Tumaini, Benedict Pius na Velasquez Severine.

Share.

About Author

Leave A Reply